Watunga sera chukueni hatua nchi zinufaike na TEHAMA- UNCTAD
Baadhi ya mataifa yanayoendelea yanaonesha uwezo wa kutumia na kuchukua teknolojia mpya ikilinganishwa na vipimo vya pato la kitaifa lakini nyingi bado zinasalia nyuma, imesema ripoti mpya ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD ya mwaka 2021 ambayo imetolewa leo Februari 25 mjini Geneva Uswisi. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.
Teknolojia hizo mpya ni zile ambazo zinatumia maendeleo ya dijitali na utandawazi ikiwemo akili bandia, mtandao wa kizazi cha sasa wa 5G uchapishaji kutumia bapa tatu au 3D, ndege zisizo na rubani na nyinginezo.