Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

WHO-Europe

WHO yatoa muongozo wa vyeti vya chanjo ya COVID-19 kielektronik

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema ingawa haliungi mkono mahitaji ya uthibitisho wa chanjo ya COVID-19 ili mtu kuweza kusafiri lakini katika mazingira mengine kulingana na tathmini ya hatari ya nchi zinazohusika, taarifa kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19 zinaweza kutumika kupunguza mahitaji ya karantini au upimaji wakati wa kuwasili katika nchi hizo. 

(Taarifa ya Anold Kayanda) 

Sauti
1'43"
UNESCO/Pornpilin Smithveja

Matumizi ya tehama yaongeza ufaulu kwa wanafunzi

Matumizi ya tehama katika kufundishia wanafunzi wa shule ya msingi nchini Kenya yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF yameongeza ufaulu wa watoto na kupunguza utoro. 

(Taarifa ya Leah Mushi( Pause)

Ni James Lokeny, mwanafunzi ya darasa la 8 katika shule ya msingi ya Namoruputh iliyoko kaunti ya Nakuru nchini Kenya akieleza kuwa hapo awali kabla ya UNICEF kuwafungia intaneti katika shule yao mawasiliano yalikuwa mabovu lakini sasa ni mazuri na wanaweza kusoma kwakupitia kompyuta ndogo au tablet.

Sauti
2'28"
© UNICEF/Sebastian Rich

Mradi wa umwagiliaji wawawezesha wakulima kutumia ardhi vizuri

Nchini Bangladesh uhaba wa maji unatishia uzalishaji wa kilimo na maisha ya wakulima hasa kutokana na kutokuwa na mifumo bora ya uwagiliaji ambayo inasababisha upotevu wa maji. Lakini sasa changamoto hizo zinageuka historia baada ya shirika la chakula na kilimo FAO kuanzisha mradi wa mifumo bora ya umwagiliaji inayotumia nishati ya jua au sola kunusuru wakulima na mazingira.

Sauti
2'37"
NASA Goddard Space Flight Center

Mhandisi kutoka Tanzaniani miongoni mwa wanawake wachache NASA

Nafasi ya mwanamke katika masuala ya sayansi, teknolojia , uhandisi na Hisabati (STEM) tukimmulika Dkt. Alinda Mashiku mhandisi katika kituo chasafari za anga cha NASA tawi la Goddard Maryland nchini Marekani, pia ni meneja anayeongoza jopo la wanaume kuhakikisha safari za satélite haziendi kombo angani. Flora Nducha amezungumza naye kupata ufafanuzi zaidi wa kazi yake na safari yake hadi kufika NASA.

Sauti
13'39"
Bethany Matta/IRIN

WFP yaomba wadau kuchangia milioni 200 kwa ajili ya Chakula nchini Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP nchini Afghanistan linatarajia kuishiwa akiba ya chakula mapema mwezi Oktoba mwaka huuu na limeomba msaada wa fedha ili liweze kusaidia mamilioni ya watu kupata mlo. 

Taarifa ya Leah Mushi ( Pause)

Video ya WFP ikionesha viunga vya mji wa Mazar, jimbo la Balkh kaskazini mwa Afghanistan, Shughuli za utoaji msaada wa chakula kwa ufadhili wa WFP zinaendelea, lengo ni kuwafikia takriban watu 500,000  wenye uhitaji.

Sauti
2'1"
© IOM 2020/Alexander Bee

UNHCR yamsaidia mkimbizi kupata elimu ya juu nchini Italia

Programu ya kimataifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na serikali ya Italia ya kuwasaidia wakimbizi kupata elimu ya juu nchini Italia imekuwa ni ngazi ya kufikia matarajio ya mkimbizi Saber ambaye kwa miaka 19 alikuwa akiishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Ethiopia. 

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA) 
Saber mkimbizi kutoka Sudan Kuisni ambaye sasa ana umri wa miaka 22 anasema  kwake bado ni kama ndoto kuweza kufika Italia na kuanza kusoma chou kikuu , ni fursa ya kipekee maishani. 

Sauti
2'22"
UNMISS/Janet Adongo

UNMISS waimarisha doria Sudan Kusini

Walinda amani wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS wanaendelea na doria ya barabarani kutoka Tambura hadi Ezo katika Jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini kutathmini hali ya usalama na kibinadamu kufuatia kuzuka kwa mzozo mkali unaoendelea katika eneo hilo. Taarifa ya John Kibego inaeleza zaidi. 

(Taarifa ya John Kibego)

Sauti
2'51"
WHO/Africa

Dkt. Tedros azikumbusha nchi za Afrika kutomsahau Mungu pamoja na kupata chanjo ya COVID19

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia mawaziri wa Afya wa Afrika wakati wanaendelea na utoaji wa chanjo ya COVID-19 wasiache kumuomba Mungu na kutumia njia za kijamii, kulikoni? Leah Mushi na undani zaidi.

Taarifa ya Leah Mushi. (Pause)

Dokta Tedros Ghebreyesus Mkurugenzi mkuu wa WHO akifungua rasmi mkutano wa 71 wa mawaziri wa Afya wa bara la Afrika.

Sauti
2'33"
© UNICEF Afghanistan

Wakimbizi 51 waki Afghan wawasili nchini Uganda

Serikali ya Uganda imethibitisha kupokea awamu ya kwanza ya wakimbizi kutoka Afghanistan asubuhi leo. Hiii ni ya kutimiza ahadi yake iliofuatia ombi la Marekani la kuhufadhi wakimbizi Zaidi ya 2,000 kutoka Afghanistan kwa muda.
Hii hapa maelezo Zaidi katika ripoti ilioandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda.


(Taarifa ya John Kibego)
Taarifa iliotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Uganda inasema kuwa raia 51 wa Afghanistani wamewasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Enteebbe asubuhi ya leo kwa za Afrika Mashariki.

Sauti
1'11"