Edwin Kinyanjui - Kutoka kuwa adui wa tembo hadi rafiki na mtetezi
Nchini Kenya kampeni ya kulinda wanyamapori nayoongozwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP imezidi kupanua wigo wake ambapo hivi sasa hata watu ambao awali walikuwa adui wa wanyamapori, wamegeuka rafiki na walinzi wakuu wa wanyama hao kama njia mojawapo ya kuhifadhi misitu kama ile ya mlima Kenya, bali pia bayonuai ambayo ni muhimu kwa viumbe vyote. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.
Katikati ya msitu mnene kwenye miteremko ya mlima Kenya tunakutana na Edwin Kinyanjui, huyu ni askari wa wanyamapori katika Wakfu wa mlima Kenya.