Nchini Uganda mafunzo ya roboti yanafungua upeo wa watoto wa Shule
Kutana na Solomon Kingi Benge mwanzilishi wa kituo cha mafunzo ya trknolojia ya roboti .Ameamua kuusambaza ujuzi wake kwa wanafunzi katika shule nchini Uganda.
Kutana na Solomon Kingi Benge mwanzilishi wa kituo cha mafunzo ya trknolojia ya roboti .Ameamua kuusambaza ujuzi wake kwa wanafunzi katika shule nchini Uganda.
Serikali ya Ecuador imetakiwa kuongeza juhudi zake ili kuhakikisha sheria inafuatwa na kutekeleza mipango ya kukomesha ubaguzi wa rangi unaowakabilia Raia weusi wa Ecuador na watu wenye asili ya Afrika.
Kenya, Musumbiji na Niger wamezuia milipuko ya ugonjwa wa polio ambayo ilishuhudiwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi 24 iliyopita na kuchangia nchi hizo kutangazwa kuwa zisizokuwa na ugonjwa wa polio kwa mujibu la tangazo la shirika la afya duniani WHO lililotolewa leo.
Kutana na Adouia mama mjasiriamali aliyefaidika na kubadili maisha yake na jamii yake kutokana na mradi wa Benki ya dunia kupitia ufadhili wa jumuiya ya kimataifa ya maendeleo (IDA).
Mwisho wa mwezi Desemba na Januari wapenda sanaa nchini Nigeria watashuhudia sanaa ya tamthilia kwa jina Bintu iliyotungwa na kuandaliwa kwa ufadhili wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na ukumbi wa maonyesho wa Mosaic.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempongeza kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kwa kupunguza madhila kwa watu na kutetea hadhi ya haki za binadamu.
Shirika la afya ulimwenguni leo limetangaza habari njema ya kupungua kwa visa vya kipindupindu duniani kote kwa asilimia 60 mwaka 2018.
Wanafunzi kote nchini Sudan Kusini wakiwemo wale wanaoishi katika vituo vya Umoja wa Usalama vya kuwahakikishia raia usalama, wanafanya mitihani ya mwisho wa mwaka ambapo mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS inafanya kazi ya kuwapeleka wanafunzi wa kambini katika shule wanakofanyia mitihani na pia kuwarejesha.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linakadiria kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya wanaume wanaotumia tumbaku imepungua ikiashiria mabadliko katika janga la tumbaku kimataifa.
Mtengenezaji wa muziki, mmarekani Jay Denton, amesafiri hadi nchini Lebanon kuandaa Albamu ya muziki kwa kushirikiana na wakimbizi wa huko kwa kuwapatia nafasi ya kupaza sauti na kueleza uzoefu wao.