Wakimbizi walio taabani Jordan waomba msaada usikatwe
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR linahitaji msaada wa haraka wa dola milioni 116 ili kuendeleza mpango wa kusaidia wakimbizi wa Syria wasiojiweza nchini Jordan.
UNHCR inasema fedha hizo zisipopatikana, italazimika kukata msaada wa fedha kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan ikiwemo walio taabani.