Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Si vita wala madhila vilivyo na dalili za kuisha Syria: Egeland

Mtoto akipita kando mwa makazi yaliyoharibiwa kwa mashambulizi kwenye moja ya vitongoji vya mji wa Aleppo nchini Syria
UNICEF/UN0145425/Charbonneau
Mtoto akipita kando mwa makazi yaliyoharibiwa kwa mashambulizi kwenye moja ya vitongoji vya mji wa Aleppo nchini Syria

Si vita wala madhila vilivyo na dalili za kuisha Syria: Egeland

Amani na Usalama

Si vita nchini Syria wala mfululizo wa madhila kwa mamilioni ya watu vilivyo na dadili ya kumalizika ameonya leo Jan Egeland akitoa taarifa kuhusu hali ya kibinadamu kwa taifa hilo lililoghubikwa na vita vya zaidi ya miaka saba sasa.

Egeland ambaye ni mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva Uswis kwamba , hofu yake kubwa ni watu kufikiria vita hivyo vimemalizika wakati ukweli ni kwamba vinaendelea na kuna maelfu kwa maelfu ya watu kutoka maeneo ya Damascuss vijijini wanajiandaa kuondoka kuelekea Idlib Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Egeland amesema hayo wakati huu kukiwa na changamoto kubwa ya kuweza kufikisha misaada ya kibinadamu katika baadhi ya maeneo , na ukata wa fedha ekiendelea kutoa changamoto kubwa ya kukidhi mahitaji. Hivyo  amewasihi wahisani kwamba “ Hadi sasa ni asilimia 23 tu ya mipango ya kibinadamu ndio iliyofadhiliwa na huu ni mwezi Mei, akionya kwamba hakuna fedha kwa wajili ya wahudumu wa kibinadamu, na maelfu ya watu wanawasili kila uchao Idlib wakiwa hoi kwa uchovu na wengine taabani wakiugua, hivyo  akasisitiza tafadhalini sana wahisani msituache hadi mchakamchaka huu wa madhila utakapokwisha.” Ameongeza kuwa

(SAUTI YA JAN EGELAND)

Idlib kwa hakika naweza kusema ndio hofu yetu namba moja, kwa sababu kwamba imejaa raia wasiojiweza . Njia moja ya kuiangalia ni kwamba ina watu mara sita zaidi ya Ghouta Mashariki , na hakujawahi kuwa na asilimia 50 ya wakimbizi wa ndani Ghouta Mashariki, wanaishi katika maeneo ya wazi, kwenye kambi za wakimbizi wa ndani zenye msongamano wakiwa wamebanana vituoni. Wanawasili saa usiku wa manane kila usiku sasa, na kukuta kwamba hawawezi hata kupata vitanda popote vinavyotolewa na wahudumu wa kibinadamu waliochoka sana. Hivyo hatuwezi kuwa na vita Idlib.”

Hadi kufikia leo watu milioni 2 bado wako kwenye maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia Syria na wengine 11,000 wanaishi katika maeneo ambayo bado yanazingirwa.