Zahma ya leo Mashariki ya Kati ina athari kwa dunia nzima:Mladenov

Manzari ya Jabalia kambi kubwa kabisa kati ya kambi 8 za a wakimbizi Ukanda wa Gaza . Ipo Kaskazini mwa Gaza karibu na kijiji cha Jabalia.
Picha na Suhair Karam/IRIN
Manzari ya Jabalia kambi kubwa kabisa kati ya kambi 8 za a wakimbizi Ukanda wa Gaza . Ipo Kaskazini mwa Gaza karibu na kijiji cha Jabalia.

Zahma ya leo Mashariki ya Kati ina athari kwa dunia nzima:Mladenov

Amani na Usalama

Hali ya Mashariki ya Kati ni tete, na inahitaji mshikamano wa pamoja kuhakikishasuluhu inapatikana na amani ya kudumu inadumishwa ili kuepusha zahma kwa dunia nzima , sasa na hata baadaye.

Zahma ya kibinadamu inayotokea leo Mashariki ya Kati ina athari kubwa kwa dunia nzima. Onyo hilo limetolewa na Nickolay Mladenov mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, akitoa taarifa kwenye baraza la uslama mjini Newy Marekani  hii leo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Amesema uingiliaji kutoka nje umebadili migogoro ya ndani na kuifanya kuwa vita vya kikanda. Akitolea mfano Syria, amesema kunashuhudiwa mashindano kati ya majeshi kadhaa ya mataifa mbalimbali, wajumbe wao, makundi mbalimbali ya upinzani yaliyojihami, wanamgambo, wapiganaji wa kigeni, na makundi kadhaa ya kigaidi.

Kisha akaugeukia mgogoro wa Israel na Palestina na kusema

Mkimbizi wa kipalestina akipokea msaada wa chakula katika eneo la Khan Younis huko ukanda wa Gaza.
UNRWA/Tamer Hamam
Mkimbizi wa kipalestina akipokea msaada wa chakula katika eneo la Khan Younis huko ukanda wa Gaza.

(SAUTI YA NICKOLAY MLADENOV)

“Ni lazima tuongeze juhudi zetu kuzisaidia pande husika kusonga mbele na mchakato endelevu wa amani baina ya Isreal na Palestina kwa misingi ya suluhu ya mataifa mawili. Matumaini ya amani yanafifia zaidi na zaidi na kuimarisha itikadi Kali, kuongeza migawanyiko na pia kutoamiana kwa pande zote.”

Mladenov ameongeza kuwa Mashariki ya Kati ni kanda ambayo imeghubikwa na migawanyiko ya kidini , ongezeko la makundi yenye itikadi Kali, ambako hasira na kiwewe haraka hugeuka ugaidi, ghasia na itikadi kali, na ni kanda ambayo vita kati ya msimamo wa wastani na itikadi kali ni vita vya mustakhbali wa mamilioni ya watu.

 

Image
Mratibu maalumu wa UM kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov. (Picha:UM/Eskinder Debebe)

Amesisitiza kuwa wakati huu mvutano ukishika kasi katika kanda nzima

(SAUTI YA NICKOLAY MLADENOV )

“Kutokuwepo na hatua zilizopigwa lazima  kututie hofu sisi wote. Moto wa Mashariki ya Kati unaendelea kuwaka ukipanua wigo wake na kuhama, na mzozo kati ya Israel na Palestina bado unasalia kuwa ni chanzo cha kuwapa uhai wanamgambo na wenye misimamo mikali kote Mashariki ya Kati.”

Hivyo amesema kuanzisha ufumbuzi wa haki, wa kina na wa kudumu wa mgogoro huo kutakata mizizi ya kutokuwa na utulivu na vurugu kutoka kanda hiyo na Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kila jitihada kutekeleza lengo hilo.