Wanasiasa acheni kueneza chuki mnaposaka wafuasi – Türk
Takribani nchi 60 duniani kote mwaka huu zikiwa zinajiandaa na chaguzi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk amezungumzia kitendo cha baadhi ya wanasiasa kuchochea ukosefu wa maelewano na chuki dhidi ya wageni kama njia ya kusaka wafuasi wa kuwaunga mkono.