Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yazipongeza Korea Kaskazini na Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM

UN yazipongeza Korea Kaskazini na Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha hatua ya Korea Kaskazini na Korea Kusini kufungua tena mawasiliano ya niia ya simu kati yao.

Hatua ya nchi hizo mbili kufungua mawasiliano ya moja kwa moja kati ya marais wao ilitangazwa Jumatano ambapo Katibu Mkuu kupitia naibu msemaji wake Farhan Haq amesema..

(Sauti ya Farhan Haq)

“Kila mara ni jambo zuri kuwa na mazungumzo kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK na Jamhuri ya Korea. Ni katika muktadha huo Katibu Mkuu anakaribisha kufunguliwa tena kwa njia za mawasiliano. Bado tunaendelea kuazimia kuhakikisha utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondokana na nyuklia kwenye rasi ya Korea.”

Halikadhalika amesema Katibu Mkuu anatumai kuwa kuimarika kwa harakati za kidiplomasia kutasaidia kufanikisha lengo hilo la kuondokana na nyuklia kwenye ukanda huo.