Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia Carlos Ruiz Massieu amesema katika kipindi cha mwaka uliopita, Colombia imeendelea kupiga hatua muhimu katika mchakato wa amani wakati ikikabiliwa na changamoto nyingi hususan katika maeneo ambako jamii imeathiriwa na vita, usalama wa viongozi wa jamii na waasi wa zamani.