Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Marekani

Mwanamume mmoja anauza mazao huko Birao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wamehamia.
© WFP/Aurore Vinot

Kumalizika kwa AGOA kutaathiri upanuzi wa mauzo ya Afrika kuelekea Marekani

Hatma ya bidhaa nyingi za kilimo na viwandani kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Marekani ipo mashakani kufuatia kumalizika kwa muda wa Mpango wa Ukuaji na Fursa za Afrika (AGOA), hatua ambayo inaweza kudhoofisha juhudi za nchi za bara hilo kupanua mauzo yao ya nje ya malighafi limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD.

Rosemary DiCarlo akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama kuhusu shambulio la Israel Doha Qatar
UN Photo/Loey Felipe

Shambulio la Israel Doha Qatar laleta mshtuko, UN yataka diplomasia iheshimiwe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo lilipewa taarifa na afisa mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu shambulio la anga la Israel mjini Doha Qatar na kusema ni ongezeko la kutisha la mvutano lililolaaniwa kama uvunjaji wa mamlaka ya nchi unaotishia mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza.

23 JUNI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini.  Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.

Sauti
10'27"
Mkuu wa IAEA Rafael Grossi amesema Jumatatu kwamba Iran haijaripoti ongezeko la viwango vya mionzi nje ya maeneo ya nyuklia ya Fordow, Isfahan na Natanz.
© IAEA/Dean Calma

Iran: Mkuu wa IAEA atoa wito wa kuruhusiwa kufika maeneo ya nyuklia yaliyoharibiwa

Baada ya mashambulizi ya ghafla ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya kurutubisha urani vya Iran mwishoni mwa wiki, mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA, linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa, leo limetoa wito wa kuruhusiwa mara moja kufika kwenye maeneo hayo ili kutathmini kiwango cha uharibifu ambacho huenda kikawa kikubwa zaidi.

Sauti
1'56"