Korea kusini

BTS yatoa video maalum, “saka upendo ndani yako uweze kusambaza kwa wengine”

Wanamuziki vijana wa kikundi mashuhuri cha muziki duniani, BTS ambao pia ni waungaji mkono wa kazi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wametoa wito kwa vijana kueneza wema katika siku hii ya leo ya kimataifa ya urafiki.

Korea yatoa tani 5,000 za chakula kwa wakimbizi, Uganda

Shrika la Mpango wa chakula duniani (WFP) nchini Uganda limekaribisha mchango tani 5,000 za mchele kutoka kwa seriakli ya Korea Kusini amabyo imeitikia mahitaji ya cahkula yanayongezeka kila uchao miongoni mwa wakimbizi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. 

Vita Yemen yageuza nchi hiyo kuwa jehanam kwa watoto- UNICEF

Yemeni hivi sasa ni jehanam ya watoto, amesema Geert Cappelaere, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Korea Kaskazini na Korea Kusini, sasa ni wakati wa vitendo halisi-Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amekaribisha matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutaon wa tatu wa mwaka kati ya viongozi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK na Jamhuri ya Korea ijulikanayo pia kama Korea Kusini.

Walinda amani Sudan Kusini wafundisha vijana stadi za kilimo cha kisasa

Hebu fikiria walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliopelekwa Sudan  Kusini kwa jukumu la kusaidia ujenzi na ukarabati wa barabara, sasa wameona wajiongeze katika usaidizi wao kwa wananchi na sasa wamefungua shamba darasa na vijana wamechangamkia mpango huo.

Msaada wa chakula kutoka Korea Kusini kukomboa wakimbizi Uganda

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), nchini Uganda limepokea kwa mikono miwili, msaada wa chakula kutoka kwa Serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya kusaidia wakimbizi katika nchi hiyo. 

Sauti -
1'6"

WFP yakaribisha msaada wa chakula kwa wakimbizi kutoka Korea Kusini

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), nchini Uganda limepokea kwa mikono miwili, msaada wa chakula kutoka kwa serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya kusaidia wakimbizi katika nchi hiyo.

 

Korea Kusini badilisha sera ya makazi- UN

Korea Kusini imeshauriwa  kubadili sera yake kuhusu  makazi na wasio na makazi ili kuweza kufikia viwango vinavyohitajika sasa vya haki za binadamu.

Uboreshaji makazi Korea Kusini waengua maskini

Nchini Korea Kusini suala la uboreshaji wa makazi duni limekuwa na madhara makubwa kwa watu wa kipato cha chini.

Maji safi kunusuru utoro wa wanafunzi Uganda

Wanafunzi 56,000 kutoka shule 100 za eneo la Karamoja, kaskazini-mashariki mwa Uganda sasa hawatokuwa na hofu tena ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama kufuatia makubaliano ya Umoja wa Mataifa na Korea Kusini. 

Sauti -
1'28"