Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Watoto wakitembea kuelekea kituo cha wakimbizi wa ndani huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan (Maktaba)
© UNICEF/Shehzad Noorani

Wasudan wangapi wafe ndio pande kinzani Sudan ziache kupigana? Ahoji Türk

Nimeshtushwa sana, kwa mara nyingine na ripoti za muaji ya kikatili ya raia kwenye kijiji cha Wad Al-Noura jimboni al Jazira nchini Sudan, Ndivyo ilivyoanza taarifa ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa haki za binadamu Volker Türk iliyotolewa leo Geneva, USwisi ikijielekeza kwenye tukio hilo la Jumatano lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 100.

Hanona Yousif Mohamed Ahmed akiwa amemleta mtoto wake Maher kwenye kituo cha lishe huko Abushok, Darfur Kaskazini, Sudan kwa uchunguzi wa afya.
© UNICEF/UN0836604/Zakaria

Kiwewe kisichofikirika chakumba wakimbizi wa ndani Sudan, huku njaa na ghasia ikitishia mamilioni

Ghasia za kutisha na hatari ya kutumbukia kwenye baa la njaa vinaendelea kunyemelea wananchi wa Sudan, yameonya mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa hii leo, wakati huo huo yakisisitizia kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kulaani shambulio kwenye Kijiji kimoja kusini mwa mji mkuu Khartoum lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Mwanamke akimlisha mtoto katika shule inayotumiwa kama mahali pa kukusanya watu waliokimbia makazi yao huko Port Sudan.
© WFP/Abubaker Garelnabei

WFP yapanua hatua za msaada wa dharura ili kuepusha njaa wananchi wanaokumbana na vita Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linapanua kwa kasi msaada wake  wa chakula cha dharura na lishe katika Sudan iliyokumbwa na vita pamoja na tishio la njaa. Halikadhalika, hali za raia zinazidi kuzorota huku mapigano yakiongezeka katika maeneo ya vita kama El Fasher na Khartoum. Hii ni kwa mujibu wa  hilo la WFP kupitia Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Michael Dunford akizungumza huko port Sudan.