Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yapanua hatua za msaada wa dharura ili kuepusha njaa wananchi wanaokumbana na vita Sudan

Mwanamke akimlisha mtoto katika shule inayotumiwa kama mahali pa kukusanya watu waliokimbia makazi yao huko Port Sudan.
© WFP/Abubaker Garelnabei
Mwanamke akimlisha mtoto katika shule inayotumiwa kama mahali pa kukusanya watu waliokimbia makazi yao huko Port Sudan.

WFP yapanua hatua za msaada wa dharura ili kuepusha njaa wananchi wanaokumbana na vita Sudan

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linapanua kwa kasi msaada wake  wa chakula cha dharura na lishe katika Sudan iliyokumbwa na vita pamoja na tishio la njaa. Halikadhalika, hali za raia zinazidi kuzorota huku mapigano yakiongezeka katika maeneo ya vita kama El Fasher na Khartoum. Hii ni kwa mujibu wa  hilo la WFP kupitia Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Michael Dunford akizungumza huko port Sudan. 

WFP inaongeza kasi ya kutoa msaada wa chakula na lishe kuokoa maisha kwa watu milioni 5 zaidi ifikapo mwisho wa mwaka huu, na kuongeza maradufu idadi ya watu ambao lilipanga kusaidia mwanzoni mwa 2024. Njaa inazidi kuongezeka nchini Sudan na katika nchi jirani ambako mamilioni ya watu wamekimbilia, na hivyo kusababisha janga la njaa ambalo linaweza kuwa kubwa zaidi duniani. 

"Janga la njaa na utapiamlo zimeikumba nchi Sudan. WFP inaendelea kupanua usaidizi wake wa chakula na lishe ili kufikia mamilioni ya watu zaidi ambao wanaishi katika hali ya tishio la vita kila siku. Hali hii tayari ni janga na ina uwezekano wa kuwa mbaya zaidi msaada usipowafikia wale wote walioathiriwa na migogoro,” amesema Michael Dunford.

Watu katika Darfur Magharibi wakipokea mgao wa dharura wa chakula.
© WFP/World Relief
Watu katika Darfur Magharibi wakipokea mgao wa dharura wa chakula.

Kama sehemu ya kuongeza msaada, WFP itatoa msaada wa pesa taslimu kwa watu milioni 1.2 katika majimbo 12. Hii inainua kwa kiasi kikubwa masoko ya ndani na wazalishaji wa chakula. WFP pia inaongeza kiasi cha chakula au fedha inachotoa kwa watu wanaokabiliwa na kiwango kikubwa cha njaa. Zaidi ya watu milioni mbili katika maeneo zaidi ya 40 yenye njaa yametambuliwa na WFP. Baadhi ya jamii katika maeneo haya, hasa katika maeneo ambayo mapigano yanaendelea, kama vile Darfurs, Kordofans, Khartoum na Gezira, wako katika hatari kubwa ya kutumbukia katika hali ya njaa iwapo hawatapata usaidizi wa haraka na endelevu.

"Hali nchini Sudan haijasahaulika sana bali  imepuuzwa. Tayari ndilo janga kubwa zaidi la watu kuhama makazi yao duniani, na lina uwezekano wa kuwa janga kubwa zaidi la njaa duniani. Wakati viongozi wa kimataifa wanazingatia mahali pengine, sudan haipati uangalizi na usaidizi unaohitajika ili kuepusha hali ya kutisha kwa watu wa Sudan. Dunia haiwezi kudai kuwa haijui jinsi hali ilivyo mbaya nchini Sudan au kwamba hatua za haraka zinahitajika,” ameongeza Dunford.

WFP inafanya kazi usiku na mchana kupanua ufikiaji na kufungua barabara mpya kwa ajlili ya misaada ya kibinadamu ili kupata usambazaji wa chakula kwa jamii katika maeneo yote ya nchi. Barara hizi zinafugunguliwa kutokea mashariki mwa Sudan kupitia Dabbah katika Jimbo la Kaskazini, kutoka Kosti hadi Kordofans, na kuvuka mipaka kutoka Chad, Misri na Sudan Kusini. WFP pia inaweka chakula mapema katika vivuko muhimu vya mpaka na njia za usambazaji bidhaa kwa sababu msimu wa mvua unaokaribia utafanya barabara za Darfurs na Kordofans kutopitika.

Nima Elmassad akiwa pichani kwenye shamba lake katika kijiji cha Um Naam Um katika jimbo la vijijini la Nile Nyeupe nchini Sudan. (Maktaba)
UNEP/Lisa Murray
Nima Elmassad akiwa pichani kwenye shamba lake katika kijiji cha Um Naam Um katika jimbo la vijijini la Nile Nyeupe nchini Sudan. (Maktaba)

Zaidi ya hayo, WFP inafanya kazi na wakulima wadogo wadogo, wengi waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro, ili kuongeza uzalishaji wa ngano. Mavuno ya kwanza yalifadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kupitia mpango huu. 

Kutokana na hali ya vita vinavyoendelea, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanajitahidi kusaidia kila mtu anayehitaji msaada. Usalama wa chakula unazidi kuzorota na unaweza kufikia viwango ambavyo havijaonekana nchini Sudan tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000. Hali kama njaa inasababishwa sio tu na ukosefu wa chakula, lakini pia ukosefu wa huduma ya matibabu na maji safi - yote haya ni hali halisi mbaya kwa wakazi wa Sudan. Watu nchini Sudan wamesalia kukata tamaa kama vile kula nyasi na majani ya mwitu ili kuishi. Utapiamlo miongoni mwa watoto nchini Sudan pia umefikia viwango vya kushangaza, na kuacha kizazi kizima katika hatari. Watoto tayari wanakufa kwa sababu zinazohusiana na utapiamlo.