Je Afrika ni tishio kubwa? Ahoji Rais Mutharika
Malawi imesema inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kutaka kuwepo kwa wajumbe wawili wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na 5 wasio na kura turufu.
Malawi imesema inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kutaka kuwepo kwa wajumbe wawili wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na 5 wasio na kura turufu.
Ukosefu wa takwimu kuhusu kilimo unazuia juhudi za kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu.
Marekani inaendeshwa na Wamarekani na ukiheshimu uhuru wetu hatutokuingilia wala kukwambia la kufanya. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Marekani Donald Trump alipouhutibia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada kutoka kwa serikali ya Korea Kusini limezindua mradi unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na huduma za kujisafi katika shule zaidi ya 100 nchini humo.
Umoja wa Mataifa na nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wa chombo hicho leo wamekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuangazia jinsi ya kuimarisha operesheni hizo.
Rais Paul Kagame wa Rwanda amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutaka kile alichokiita kuwa maendeleo chanya barani Afrika kisipuuzwe licha ya changamoto zinazokumba bara hilo.
Misingi mikuu mitatu ambayo ni uongozi bora, kushirikiana majukumu na kuchukua hatua za pamoja ni muhimu kwa mustakhbali wa dunia amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Espinosa.
Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 umefunguliwa rasmi hii leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wawakilishi kutoka nchi 193 wanachama, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo wakikutana kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa inatimia ifikapo 2030.
Madiliko kuhusu suala la uhamiaji barani Afrika ni lazima, kwani yatasaidia kwanza kubadili fikra na mtazamo kuhusu suala la uhamiaji, lakini pia kusongesha mbele gurudumu la maedeleo endelevu au SDG’s kwa mataifa ya bara hilo.
Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo, wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wanakutana kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto za ulinzi wa amani.