Tuepushe mapigano CAR, hali ni tete- Zeid
Ghasia zinazidi kupamba moto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR jambo ambalo linamtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein.
Ghasia zinazidi kupamba moto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR jambo ambalo linamtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein.
Hadi kufikia sasa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linaweza kuthibitisha kuwa ahadi zinazohusiana na nyuklia zinatekelezwa na Iran.
Baada ya kupoteza kila kila kitu wakati wa migogoro wa kivita nchini kwao Burundi , mwanamke mkimbizi aliyekimbilia Rwanda anasema , hajutii mali na vitu alivyovipoteza kwani yeye na familia yake wapo salama aliko ukimbizini.
Mtoto mmoja raia wa Syria ambaye amekuwa akikimbia vita kwa miaka mitano sasa bado hajaweza kupata unafuu kwa kuwa kila aendako ikiwemo nchini Libya bado hali ni ngumu.
Guterres ataka shaka na shuku kwenye JCPOA iondolewe kwa kuzingatia mfumo uliowekwa na si kwa pande husika kujitoa kwenye makubaliano hayo yanayolenga kuwezesha Iran kuachana na nyuklia.
Shirika la afya ulimwenguni WHO linaendelea na juhudi za kuwalinda wakimbizi wa Rohingya karibu milioni moja nchini Bangladesh dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, huku leo likionya kwamba hatari bado ipo.
Ebola yabisha tena hodi DRC, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu mlipuko mwingine utokee nchini humo kipindi kama hiki na kudhibitiwa baada ya miezi mitatu.
Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea hofu yao kuhusu kuendelea kushikiliwa rumande kwa mwandishi wa blogu wa Mauritania Cheikh Ould Mohamed M’kheitir kwa mdai ya kukiuka haki za binadamu.
Umoja wa Mataifa umetaka nchi wanachama zitumie vyema mafaniko yanayoibuka na kile kinachoitwa mapinduzi ya nne ya viwanda duniani.
Licha ya mafanikio yaliyoshuhudiwa katika miaka 20 iliyopita , takwimu mpya za shirika la kazi duniani ILO zinaonyesha kuendelea kwa pengo la kutokuwepo usawa kati ya wanawake na wanaume katika soko la ajira, kutokuwa na kazi na mazingira ya kazi.