Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa Ebola DRC watokomezwa- WHO

Mlipuko wa Ebola DRC watokomezwa- WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa hivi karibuni zaidi wa ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Tangazo hilo linafuatia kutokuwepo kwa kisa kipya cha Ebola ndani ya siku 42 tangu kisa cha mwisho kiripotiwe kwenye jimbo la Bas-Uélé.

Tarehe 11 mwezi Mei mwaka huu WHO ilijulishwa kuhusu visa vya ebola kwenye eneo la Kikati ambapo watu wanne walifariki dunia na wanne walipona.

Huu ni mlipuko wa Nane wa Ebola nchini DRC tangu mwaka 1976.