Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita vimewafukuza kwao na hata ugenini

Milio ya silaha nzitonzito kama hizo mjini Misrata Libya ilimuathiri mtoto Bassam mwenye umri wa miaka 8. Ataka warejee nyumbani Syria.
Picha ya OCHA
Milio ya silaha nzitonzito kama hizo mjini Misrata Libya ilimuathiri mtoto Bassam mwenye umri wa miaka 8. Ataka warejee nyumbani Syria.

Vita vimewafukuza kwao na hata ugenini

Amani na Usalama

Mtoto mmoja raia wa Syria ambaye amekuwa akikimbia vita kwa miaka mitano sasa bado hajaweza kupata unafuu kwa kuwa kila aendako ikiwemo nchini Libya bado hali ni ngumu.

Nats

Ni mtoto Bassam mwenye umri wa miaka minane akisema kuwa hawezi kurejea Misrata kwa kuwa kuna vita. Anasema angetaka warejee nchini mwao Syria.

Bassam na familia yake akiwemo baba, mama na nduguze walikuwa Misri kwa matibabu wakati vita vinaanza nchini Syria.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, familia hii ilihamia Libya kusaka maisha ambako nako hali si shwari.

Kila mara milio ya risasi bila kusahau vitendo vya kikatili kutoka kwa makundi yaliyojihami.

Baba mzazi wa Bassam, Ali Muhammed anasimulia ukatili alioshuhudia mwanae.

(Sauti ya Ali Muhammed)

“Walifunga mwili wa mwanadamu nyuma ya gari na kuuvuta  kupitia barabara kuu na Assam aliona hiyo. Kwa sasa kila mara huamka kutoka usingizini akiwa na uoga.”

Vita na umaskini vimemuathiri mtoto huyu na sasa amekondeana akiwa na uzito wa chini ya kilo 20 huku mwenye akikumbuka uzito wake wa awali.

(Sauti ya Bassam)

“Nilikuwa na kilo 27. Inafaa tuondoke hapa.”

Bwana Muhammed anataka wahamie Ulaya akiamini kuwa huko maisha ni bora kuliko Libya hata hivyo wanahofia kuvuka baharí ikizingatia taarifa nyingi zinazoonyesha watu wakifa majini.