Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sijutii kupoteza mali zangu ilimradi familia yangu ipo salama

Picha ya UN women
Mama na mtoto katika kambi wa wakimbizi Rwanda

Sijutii kupoteza mali zangu ilimradi familia yangu ipo salama

Wahamiaji na Wakimbizi

Baada ya kupoteza kila  kila kitu wakati wa  migogoro wa kivita nchini kwao Burundi , mwanamke mkimbizi aliyekimbilia Rwanda  anasema , hajutii mali na vitu alivyovipoteza  kwani yeye na familia yake wapo salama aliko ukimbizini.

Huyu ni Bi Marai katika video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa lengo la kupigia chepuo wanawake madhubuti.

Bi Marai ambaye sasa anaishi kambi ya  mahama nchini  anasema yeye, mumewe  na watoto wawili,  Vestine mwenye umri wa miaka 5 na Zahaka mwenye umri wa mwaka mmoja wapo salama.

Sauti ya Marai

"Nilipokimbia vita, sikuja na kitu chochote, niliacha kila kitu huko nyumbani. Ila kwa sababu niko na mume wangu na watoto wangu, sipungukiwi na chochote.”

Marai kama wanawake wengine kambini alikimbia machafuko huko nyumbani kwao Burundi akiwa mjamzito.

Amesema walipofika Rwanda alipokelewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR na kupatiwa huduma ambapo alijifungua salama hapo kambini.

Katika kuelekea siku ya mama duniani mwezi huu wa Mei, Bi Marai anawatakia wanawake wote katikakambi za wakimbizi na duniani kote mafanikio katika kuzihudumia familia zao.