Hatari bado ipo kwa wakimbizi takriban milioni 1 wa Rohingya: WHO

8 Mei 2018

Shirika la afya ulimwenguni WHO linaendelea na juhudi za kuwalinda wakimbizi wa Rohingya karibu milioni moja nchini Bangladesh dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, huku leo likionya kwamba hatari bado ipo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO linaendelea na juhudi za kuwalinda wakimbizi wa Rohingya karibu milioni moja nchini Bangladesh dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, huku leo likionya kwamba hatari bado ipo.

Dkt. Richard Brennan, mkurugenzi wa operesheni za dharura wa WHO ametoa onyo hilo mjini Geneva Uswisi akielezea hatari za magonjwa mengine , majanga ya asili na upungufu mkubwa wa fedha.

Amesema idadi kubwa ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh wanaishi katika kambi zilizofurika na chafu, na sasa kuna tishio lingine la mafurko, maporomoko ya udogo na msimu wa vimbunga.

Dkt.Brennan ameongeza kuwa sasa kampeni ya chanjo ya kipindupindu inaendelea na ni ya muhimu kama awamu ya pili baada ya ile ya Oktoba na Disemba mwaka jana.

Licha ya tishio hilo , WHO inasema kipindupindu ni hofu moja ya kiafya miongoni ma masuala mengi ya kuyapa kipaumbele, ikisistiza kwamba kuna haja ya kujikita katika suala la maji na vifaa vya usafi vikiwemo vyoo kama hakikisho la kudhibiti magonjwa mengine ya mlipuko yatokanayo na maji.

Tatizo lingine kubwa kwa mujibu wa WHO ni upungufu wa fedha ambapo kati ya dola milioni 950 zinazohitajika ni asilimia 16 tu iliyopatikana huku huduma za afya zikumbwa na mtihani mkubwa zaidi kwani mahitaji yake yametimizwa kwa  asilimia 6.3 pekee.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter