Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UNHCR yahimiza mapigano yakomeshwe Kivu Kaskazini kunusuru raia

Antonio Gutteres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ambaye alizuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK)hivi karibuni, ametoa mwito wenye kuyanasihi makundi yote yalioshiriki kwenye uhasama na mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo, hali ambayo ikikamilishwa itayawezesha mashirika ya kimataifa yanayofadhilia misaada ya kiutu kupata fursa ya kuhudumia kihali umma muhitaji ulionaswa kwenye mazingira ya mapigano.

Wanafunzi wa Kenya kutuma kadi za kufarijia walinzi wa amani wananchi

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba wanafunzi wa skuli kadha za Kenya, hivi karibuni waliwatumia wanajeshi wananchi 1,100 ziada, wanaoshiriki sasa kwenye operesheni nane za ulinzi wa amani za UM kadi za Noeli na Mwaka Mpya 2000, ikiwa miongoni mwa juhudi za kuwatoa kwenye upweke na kuwaliwaza ili nawo washereheke kama inavyotakiwa Siku Kuu za mwisho wa mwaka.

Ya hapa na pale

Miaka 15 baada ya kuanzishwa majadiliano ya kusailia taratibu za kuhifadhi misitu ya dunia na uharibifu, Baraza Kuu la UM limefanikiwa kupitisha azimio la khiyari litakalosaidia kuimarisha hifadhi bora ya hii rasilmali ya kimataifa.

Kumbukumbu ya khatima ya Mkutano wa Bali juu ya Mabadiliko ya Hewa Duniani

Viongozi wa kisiasa kutoka mataifa 180 ziada waliokusanyika kisiwani Bali, Indonesia kwa muda wa wiki mbili kwenye Mkutano juu ya Udhibiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani walifanikiwa Ijumamosi kugongolea makubaliano ya mfumo wa kuanzisha majadiliano ya kuwasilisha mkataba muhimu wa kimataifa kupabamana na athari za kimazingira, zinazochochewa na muongezeko wa joto ulimwenguni.

Ripoti juu ya shambulio la ofisi za UM Algeria

Ijumanne, tarehe 11 Disemba ofisi ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) iliopo mjini Algiers, Algeria iliharibiwa na kuporomoshwa baada ya kuekewa bomu lililosababisha vifo vya watu 14 pamoja na idadi kadha ya majeruhi.