Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mazungumzo ya amani kwa Darfur yafanyika Khartoum

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani kwa Sudan (UNMIS) limeripoti kuwa Alkhamisi kulifanyika mkutano wa sita wa Utaratibu wa Amani wa Sehemu Tatu, katika mji wa Khartoum, Sudan ambapo kulijumuika wawakilishi wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani vya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU), wawakilishi wa UM pamoja na wale wa Serekali ya Sudan ambao walizingatia, kipamoja, furushi la mapendekezo ya kuimarisha zaidi operesheni za amani za vikosi vya AU katika Darfur.

MONUC imethibitisha askari watoto wanaendelea kuajiriwa DRC, kinyume na kanuni za kimataifa

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUC)limethibitisha kwenye ripoti yake iliobainishwa wiki hii, ya kuwa askari watoto, wenye umri mdogo, bado wanaendelea kushinikizwa kusema uongo kuhusu umri wao na hadhi yao ya kiraia, ili wapate fursa ya kujiandikisha na jeshi jipya la muungano la taifa. TRukio hili limeshuhudiwa kujiri katika jimbo la Kivu Kaskazini.

WFP kununua chakula Msumbiji kuhudumia waathiriwa wa mafuriko

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa mwito wa kufadhiliwa, kidharura, msaada wa fedha zinazohitajika kununua chakula kutoka Msumbiji, taifa liliodhurika na mafuriko kusini ya Afrika. Lengo la hatua hii ni kunusuru maisha ya raia muhitaji 120,000 walioathiriwa na mafuriko yalizka hivi karibuni katika taifa hilo.

Mkuu wa UNESCO anashtumu unyanyasaji wa wanahabari Eritrea

Koichiro Matsuura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ameripotiwa akisema ya kwamba hakuridhika hata kidogo juu ya namna waandishi habari wanavyotendewa na wenye madaraka katika Eritrea na vikwazo walioekewa vyombo vya habari dhidi ya uhuru wa kuendeleza kazi zao bila ya kuingiliwa na serekali.