Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Baraza la Usalama latathminia amani na usalama wa Afrika

Viongozi wa Kitaifa, wakijumuika na wakuu wa Serekali pamoja na mawaziri wa vyeo vya juu kutoka nchi 15 zilizo wanachama wa Baraza la Usalama, pamoja na KM wa UM Ban Ki-moon na Mwenyekiti Alpha Oumar Konare wa Umoja wa Afrika (AU) walikusanyika mapema wiki hii kwenye Baraza la Usalama kujadilia njia bora za kurudisha utulivu wa amani na usalama katika Afrika, eneo ambalo linadaiwa kuwa na vurugu na migogoro ya kila aina.

Baraza Kuu laanza rasmi mjadala wa wawakilishi wote

Ijumanne, tarehe 25 Septemba (2007) wajumbe wa kimataifa walianza rasmi mahojiano ya mwaka kwenye kikao cha wawakilishi wote kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la UM. Kikao cha mwaka huu ni cha 62, na wajumbe kutoka Mataifa Wanachama kadha wa kadha waliwasilisha sera zao za kitaifa kuhusu hatua wanazochukua kukabiliana na matatizo yanayosumbua walimwengu.~~Raisi mpya wa Baraza Kuu, Srgjan Kerim, kutoka Jamhuri ya Yugoslavia ya Zamani ya Macedonia pamoja na KM wa UM, Ban Ki-moon walijumuika na viongozi mbalimbali wa Nchi Wanachama kuzingatia taratibu za kuchukuliwa kipamoja kustawisha uhusiano mwema wa kimataifa.

WFP kununua mahindi Lesotho kusaidia Liberia

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kununua mahindi kutoka wakulima wadogo wadogo wa Lesotho, mahindi ambayo yatatumiwa kuwapatia chakula na lishe bora kwa maelfu ya watoto wa skuli za praimari katika Liberia.

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali kuzuru Mogadishu

Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Usomali, Ahmed Ould Abdallah karibuni alifanya ziara rasmi Mogadishu na kuwa na mazungumzo na viongozi wa Serekali ya Mpito, wakiwemo Raisi na Waziri Mkuu. Abdallah kwenye majadiliano yake aliyahimiza makundi yote husika na mgogoro wa Usomali kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya ule mwafaka wa Mkutano wa Upatanaishi wa Taifa.