Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Juhudi za kimataifa kupiga vita utekaji nyara wa watoto Afrika

Majuzi wawakilishi wa mataifa zaidi ya 10 kutoka Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu walikusanyika mjini Kampala, Uganda kwenye mkutano wa Shirika la UM dhidi ya Jinai na Madawa ya Kulevya (UNODC), na walizingatia ratiba ya sheria imara dhidi ya biashara ya magendo ya kuteka nyara watu na watoto, na kuwavusha mipaka kutoka makwao na kuwapeleka kwenye maeneo mengineyo kuendeleza ajira haramu, ya lazima, inayotengua kabisa haki za kibinadamu.~~

Baraza la Usalama laarifiwa na H. Annabi ratiba ya vikosi vya mseto kwa Darfur

Wiki hii Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha faragha kusikiliza ripoti ya Hedi Annabi, Naibu Mkuu wa Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani ambaye alielezea kuhusu ratiba ya siku zijazo inayotakikana kutekelezwa ili kuharakisha upelekaji wa kile kinachojulikana kama ‘furushi zito’ la vikosi vya mseto vya UM na AU katika Jimbo la Darfur, Sudan. Annabi alisisitiza kwenye risala yake juu ya jukumu adhimu la jumuiya ya kimataifa kuikamilisha kadhia hiyo ya amani kidharura.

Taarifa juu ya hali Usomali

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Usomali imeelezea maelfu ya raia bado wanaendelea kuhajiri mji mkuu wa Mogadishu katika mwezi Juni, kwa sababu ya kufumka tena mapigano.