Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuanzisha taadhima za mwaka kuheshimu miaka 60 ya Azimio la Haki za Binadamu

UM kuanzisha taadhima za mwaka kuheshimu miaka 60 ya Azimio la Haki za Binadamu

Tarehe 10 Disemba huheshimiwa kila mwaka kama ni ‘Siku Kuu ya Kuadhimisha Haki za Binadamu Kimataifa’, siku ambayo ilipendekezwa baada ya Baraza Kuu la UM lilipopitisha Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu tarehe 10 Disemba 1948.

Siku Kuu ya Haki za Binadamu kwa 2007 ilipewa mada iliotilia mkazo “heshima na haki kwa wote” na mnamo tarehe 10 Disemba UM ulianzisha kampeni maalumu, itakayoendelea mwaka mzima, itakayoyajumuisha taasisi na mashirika ya UM kwenye huduma za kuelimisha na kuamsha hisia za walimwengu juu ya umuhimu wa Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, ambalo linatarajiwa kutimiza miaka 60 tangu kupitishwa katika tarehe 10 Disemba 2008.

Raisi wa Baraza Kuu la UM, Srgjan KERIM alikumbusha kwenye risala yake kwamba ni “wajibu wetu sote kuhakikisha tunatetea, bila pingamizi, haki halali za binadamu kwa wote, na kuhakikisha wanadamu wote wanaonyimwa haki hizo duniani wanatekelezewa kimataifa halan.”

Risala ya KM wa UM Ban Ki-moon kuiadhimisha Siku Kuu ya Haki za Binadamu ilisisitiza kwamba uhuru uliodhukuriwa na kuzingatiwa ndani ya Azimio la Kimataifa Kutetea Haki za Binadamu umedhamiriwa kunufaisha na kufurahiwa na kila mtu, pote ulimwenguni na sio wachache wa tabaka fulani katika jamii ya kimataifa.

Salamu za Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour zilitilia mkazo umuhimu wa kuwepo chombo cha kimataifa kama hicho kulinda haki za binadamu kwa wote. :

Armando Swenya, akiwakilisha shirika lisio la kiserekali la STARINGON, Tawi la Tanzania alielezea namna umma wa Afrika Mashariki unavyoiheshimu Siku Kuu hii.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.