Wanafunzi wa Kenya kutuma kadi za kufarijia walinzi wa amani wananchi

Wanafunzi wa Kenya kutuma kadi za kufarijia walinzi wa amani wananchi

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba wanafunzi wa skuli kadha za Kenya, hivi karibuni waliwatumia wanajeshi wananchi 1,100 ziada, wanaoshiriki sasa kwenye operesheni nane za ulinzi wa amani za UM kadi za Noeli na Mwaka Mpya 2000, ikiwa miongoni mwa juhudi za kuwatoa kwenye upweke na kuwaliwaza ili nawo washereheke kama inavyotakiwa Siku Kuu za mwisho wa mwaka.

Kadi hizo zilitengenezwa na wanafunzi wenyewe na zitawahamasisha kustarehea vizuri shamrashamra za Noeli na Mwaka Mpya wale wanajeshi walio mbali na aila zao.