Ripoti juu ya shambulio la ofisi za UM Algeria

Ripoti juu ya shambulio la ofisi za UM Algeria

Ijumanne, tarehe 11 Disemba ofisi ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) iliopo mjini Algiers, Algeria iliharibiwa na kuporomoshwa baada ya kuekewa bomu lililosababisha vifo vya watu 14 pamoja na idadi kadha ya majeruhi.

Mkuu wa Shirika la UNDP, Kemal Dervis pamoja na mkuu wa Idara ya [UM juu ya] Ulinzi na Usalama waliwasili mjini Algiers wiki hii baada ya KM Ban Ki-moon kuamua kuwapeleka huko kusailia hali halisi ya maafa hayo. Bw Dervis Alkhamisi alizuru aila za waathiriwa pamoja na kuzuru hospitali ambapo walipelekwa watumishi wa UM waliojeruhiwa na ajali ya bomu kufanyiwa matibabu. Bw Dervis alikumbusha “waathiriwa wa ajali hiyo hawakuwa wanajeshi waliojiandikisha kupigana, bali fungu kubwa lao walikuwa wazaloendo wa Algeria, waliojitolea kuenedelza huduma za amani, kukuza maendeleo na kupunguza usumbufu wa kimaisha kwa umma.”