Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu ya khatima ya Mkutano wa Bali juu ya Mabadiliko ya Hewa Duniani

Kumbukumbu ya khatima ya Mkutano wa Bali juu ya Mabadiliko ya Hewa Duniani

Viongozi wa kisiasa kutoka mataifa 180 ziada waliokusanyika kisiwani Bali, Indonesia kwa muda wa wiki mbili kwenye Mkutano juu ya Udhibiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani walifanikiwa Ijumamosi kugongolea makubaliano ya mfumo wa kuanzisha majadiliano ya kuwasilisha mkataba muhimu wa kimataifa kupabamana na athari za kimazingira, zinazochochewa na muongezeko wa joto ulimwenguni.

Maafikiano ya Mkutano wa Bali yalichelewa kukamilishwa kwenye ile siku ilyoandaliwa kumaliza majadiliano, yaani Ijumaa ya tarehe 14 Disemba. Mkutano huo ulilazimika kuongeza siku moja zaidi ambapo wajumbe wa kimataifa walipata fursa ya kuwasilisha mwafaka wa kuridhisha; na ilipofika saa nane na nusu kwa majira ya Bali, Indonesia katika Ijumamosi ya tarehe 15 Disemba, makubiliano yalikamilishwa na mwafaka wa kuridhisha ulifikiwa na nchi wanachama, baada ya kuzuka mizungu na misokoto kadha wa kadha ambayo iliwasumbua wajumbe wa kimataifa kwa wiki mbili mfululizo, hususan wale wawakilishi wa kutoka mataifa yanayoendelea.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.