Kwa ujumla usalama umerejea Burundi na wakimbizi wanarudi: Nibigira
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi amesema kwa ujumla hali ya usalama na utulivu imerejea Burundi na kilichosalia ni matukio madogomadogo ya utovu wa nidhamu.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi amesema kwa ujumla hali ya usalama na utulivu imerejea Burundi na kilichosalia ni matukio madogomadogo ya utovu wa nidhamu.
Mwaka jana nilisimama mbele yenu nikiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi iliyogubikwa na vita. Leo hii nimesimama tena mbele yenu kama shuhuda wa kile ambacho wanachama wa chombo hiki adhimu wamesaidia kufanikisha ndani ya Jamhuri ya Sudan Kusini.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema lina wasiwasi kuhusu usalama wa maelfu ya raia katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ambako ghasia za makundi yenye silaha zimeongezeka na za hivi karibuni zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 20. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
Suala la uhamiaji likiendelea kuibua vuta nikuvute, Msumbiji imesema kuwa la msingi ni watu kufuata sheria kwani uhamiaji umekuwepo na utaendelea kuwepo.
Katika kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu SDGs, Kenya imezindua mpango maalum wa mambo manne makuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo ambayo ukomo wake ni 2022.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesema imeamua kutoshiriki mkutano maalumu wa ngazi ya juu wa mawaziri ulioandaliwa kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala yanayolighubika eneo la Afrika ya Kati ikiwemo DRC.
Ukosefu wa usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo barani Afrika, unakwamisha maendeleo ya kutokomeza njaa barani humo, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa Jose Graziano da Silva.
Tanzania itatumia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kutangaza msimamo wake na chombo hicho chenye wanachama 193. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
Kenya imesema inauchukulia kwa uzito wa juu mkutano wa leo wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs, kutokana magonjwa hayo kuathiri baadhi ya wananchi wake.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametaka mshikamano na hatua kali kutoka kwa baraza hilo dhidi ya silaha za maangamizi zikiwemo za nyuklia, kibaolojia na za kemikali.