Uhamiaji sio shida Afrika la msingi kutovunja sheria- Rais Nyusi
Suala la uhamiaji likiendelea kuibua vuta nikuvute, Msumbiji imesema kuwa la msingi ni watu kufuata sheria kwani uhamiaji umekuwepo na utaendelea kuwepo.
Uhamiaji sio mzigo wala shida, unageuka kuwa shubiri pale sheria zinapovunjwa au watu kuitumia vibaya fursa hiyo kwa vitendo vya kihalifu. John Kibego na taarifa kamili
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alipozungumza na idhaa ya Kiswahili wakati wa mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York Marekani na kujadili nada mbalimbali ikiwemo uhamiaji.
Rais Nyusi ambaye pia ameishukuru serikali ya Kenya kwa kuwakumbatia raia wa Msumbiji waliokuwa wahamiaji wa miaka mingi nchini humo amesema Afrika hivi sasa imebadilika na kuwa na mtazamo chanya kuhusu uhamiaji na faida zake.
Ameongeza kuwa hata nchi yake haijafunga mipaka wala milango kwa wahamiaji
(SAUTI YA RAIS FILIPE NYUSI )