Ukarabati na ujenzi wa Ukraine utahitaji dola bilioni 486 katika muongo ujao: UN
Ujenzi mpya na ukarabati baada ya vita nchini Ukraine unakadiriwa kugharimu dola bilioni 486 katika muongo ujao, kutoka dola bilioni 411 zilizokadiriwa mwaka mmoja uliopita, umesema utafiti uliochapishwa leo ambao umeungwa mkono na Umoja wa Mataifa.