Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi ya kikatili dhidi ya raia Ukraine lazima yakome: Brown

Urusi inaendelea kulipua miji ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kyiv (pichani).
© UNOCHA
Urusi inaendelea kulipua miji ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kyiv (pichani).

Mashambulizi ya kikatili dhidi ya raia Ukraine lazima yakome: Brown

Amani na Usalama

Nchini Ukraine mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu wa nchi hiyo Denise Brown amelaani vikali wimbi jipya la mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya miji iliyo na watu wengi nchinihumo.

Katika taarifa yake iliypotolewa leo mjini Kyiv Bwana Brown amesema asubuhi ya leo “ Nilikuwa nakunywa kahawa nyumbani Kyiv, majirani zangu walikuwa wakijiandaa kwenda kazini, watoto wakijiandaa kwenda shuleni, wakati nyumba zetu zilianza kutikisika kwa sababu ya wimbi la mashambulizi ya anga kwenye mji mkuu wa Ukraine. Mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu wa majengo ya raia karibu na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Kyiv. Nyumba ziliharibiwa na raia wale niliowataja ambao walikuwa wakijaribu tu kuendelea na maisha yao licha ya vita sasa wamelazwa hospitalini. Mashambulzi haya dhidi ya raia lazima yakome.

Ameongeza kuwa huko Kharkiv, timu yetu iliyoko huko imetuambia kuwa waokoaji wanajaribu kutafuta watu waliofukiwa chini ya vifusi vya jengo la makazi lililosambaratishwa na wimbi la mashambulio ya anga pia limesababisha hasara na uharibifu katika mkoa wa Dnipro.

Amesisitiza kuwa mashambulizi haya bado ni ukumbusho mwingine mchungu wa uharibifu, mateso na dhiki ambayo uvamizi wa Urusi unasababisha kwa mamilioni ya watu nchini Ukraine.

Mashambulizi ya kikatili na ya kiholela dhidi ya raia lazima yakome.