Siku ya elimu duniani, UNESCO yasema mwamko katika ushirikiano kimataifa wahitajika kufanikisha SDG4
Leo Januari 24 ni siku ya kimatifa ya elimu duniani ambayo inaadhimishwa kwa mara ya kwanza tangu kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Desemba mwaka jana kwa kutambua umuhimu wa elimu katika kubadili dunia na kufikia ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.