Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi kutoa Syria sasa dereva wa mabasi ya umma Berlin

Wafanyakazi wahamiaji kutoka Moldova wakiwa kwenye ubomoaji wa majengo huko Podolsky mjini Moscow,  nchini Urusi
ILO/Marcel Crozet
Wafanyakazi wahamiaji kutoka Moldova wakiwa kwenye ubomoaji wa majengo huko Podolsky mjini Moscow, nchini Urusi

Mkimbizi kutoa Syria sasa dereva wa mabasi ya umma Berlin

Wahamiaji na Wakimbizi

Mataifa yameendelea kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kujumuisha wakimbizi na wahamiaji kwenye jamii zao ambapo mfano wa hivi karibuni zaidi ni mji wa Berlin nchini Ujerumani ambapo wakimbizi wakiwemo kutoka Syria wamepatiwa mafunzo ya kuendesha mabasi ya usafiri wa umma. 

Mji wa Berlin nchini Ujerumani, harakati za kila siku zikiendelea ambapo magari ya usafiri wa umma yapo kwenye pilikapilka za kuwasafirisha abiria. Cha kutia moyo ni kwamba miongoni mwa madereva wa mabasi haya ni mkimbizi Al Said kutoka Syria ambaye anaonekana akitembea kuelekea kwenye basi aendeshalo.

Mkimbizi huyu mwenye umri wa miaka 33 alisomea Kiarabu na alikuwa na ndoto za kuwa mwalimu lakini vita nchini Syria vilimsukuma hadi ukimbizini.

Ndoto za kuwa mwalimu zilitumbukia nyongo lakini lipowaambia kwamba aliwahi kuwa dereva nchini mwake wakamuomba awasiliane na halmashauri ya usafiri mjini Berlin na hatimaye akapata mafunzo ya mwaka mzima.. 

“Kile ninachokipenda kuhusu kazi yangu ya kuendesha basi ni kuhudumia watu, kuwasafirisha wazee kutoka sehemu moja hadi nyingine, kuwasaidia watu ni jambo muhimu ambalo nalifanya kila siku.”

Licha ya kuwa ukimbizini  lakini kazi aliyoipata imebadili maisha yake na familia yake ya watoto wawili ambapo anasema,

“Kazi hii kama dereva wa basi ni muhimu sana kwangu sasa, imenilietea usalama huku Ujerumani na inamaanisha kuwa ninaweza kukidhi mahitaji ya familia yangu. Na hiyo ni muhimu sana kwangu.”