Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi utafanyika mwaka huu DRC kama ilivyopangwa:Kabila

Rais Joseph Kabila wa DRC mapema mwaka huu akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 mjini New York Marekani aliuhakikishia mkutano huo kuwa kwa vyovyote vile uchaguzi nchini mwake utafanyika kama ulivyopangwa.
UN Photo/Cia Pak

Amani na Usalama

Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu hautobadilishwa utafanyika kama ilivyopangwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo wakati akihutubbia mjada wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 mjini New York Marekani.

Ameongeza kuwa kila juhudi itafanyika “kuhakikisha uchaguzi wa amani na wa kuaminika, hakikisho la kuleta utulivu wa kisiasa na kiuchumi , jambo ambalo DRC inalihitaji kwa hamu na gamu na haraka.”

Akigeukia mada ya mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa Rais Kabila amesema, haitowezekana kuufanya Umoja huo kuwa “shirika la wote” endapo “hali ya kuzivumilia baadhi ya nchi kuingilia siasa za ndani za mataifa mengine bila kuchukuliwa hatua”

Amefafafanua msimamo wa DRC kuhusu suala hilo na kusema kuwa “inapinga vikali uingiliaji wa aina yoyote ile katika mchakato wa uchaguzi unaoendelea”

Kwa mara nyingine Rais Kabila ameelezea dhamira ya taifa lake la DRC kutaka mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, kuondoka baada ya kuwemo kwa takribani miongo miwili na kusisitiza “Miaka 20 baada ya vikosi vya Umoja wa Mataifa kuwasili nchini mwangu na sababu ya matokeo makubwa , serikali yangu inarejea madai yake ya kutaka Umoja wa Mataifa kuanza kuondoa vikosi vyake  DRC.”