Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Dola milioni 675 zahitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona:WHO
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus, leo Jumatano ametoa ombi la dola milioni $675 million ili kupiga jeki hatua za kimataifa za kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona wakati idadi ya vifo kutokana na homa hiyo ikikaribia 500.
WHO yajizatiti kukabiliana na taarifa potofu kuhusu virusi vya corona, Guteress aonya kuhusu unyanyapaa
Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limechukua hatua kuhakikisha kuwa janga la virusi vya corona ambalo limesababisha vifo vya mamia ya watu katikati mwa China halitachangia kuchochewa kwa taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii.
Tukijitolea zaidi kupambana na corona, matokeo yanaweza kuwa mazuri-WHO
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus hii leo akihutubia mkutano wa 146 wa bodi kuu ya shirika hilo mjini Geneva Uswisi ameeleza hatua iliyofikiwa hivi sasa kuhusu hali ya ugonjwa wa virusi vya corona.
Msiwanyanyapae watu wa asili ya Asia kwa sababu ya corona-UN
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutowanyanyapaa na kuwabagua watu wenye asili ya bara Asia kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona ambavyo vimeathiri kwa kiasi kikubwa China na nchi nyingine.
Tuko tayari kusaidia kiufundi katika mlipuko wa corona:IOM
Wakati hofu ikiendelea kutanda kuhusu idadi ya visa vilivyoripotiwa kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya Corona na pia kusambaa kwake katika nchi 18 hivi sasa, shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema liko tayari kutoa msaada wa kiufundi kwa serikali likishirikiana na shirika la afya ulimwenguni WHO ili kuwawezesha watu kusafiri katika njia salama kiafya na kusaidia utekelezaji wa hatua za afya za kijamii ili kuhakikisha athari ndogo katika jamii na uchumi.
Kenya kuhakikisha kuna mikakati endapo Virusi vya Corona vitazuka:WHO
Shirika la afya ulimwenguni WHO limeendelea kuzitaka nchi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa dhidi ya virusi vya corona ambavyo tayari vimetangazwa kuwa dharura ya afya ya kimataifa vitazuka katika nchi zao.
31 JANUARI 2020
Jaridani Januari 31, 2020 na Arnold Kayanda. Ikiwa leo ni Ijumaa utasikia Habari kwa ufupi, mada kwa kina imejikita katika mlipuko wa virusi vya corona tukiangazia nchini Kenya ambako kuna mgonjwa anayefanyiwa uchunguzi kuthibitisha iwapo ana virusi vya corona baada ya kuwasili kutoka China na dalili za homa. Na ikiwa leo ni Ijumaa tutasikia uchambuzi wa neno la wiki kutoka BAKITA.
Virusi vya Corona sasa vyatangazwa kuwa dharura ya kiafya ya kimataifa
Mkutano wa pili wa kamati ya dharura ulioitishwa hii leo mjini Geneva Uswisi na shirika la afya duniani, WHO, chini ya sheria za kimataifa za afya (IHR) (2015) kuhusiana na mlipuko wa virusi vya corona 2019-nCoV nchini China, umeutangaza mlipuko huowa virusi vya corona kuwa ni dharura ya kiafya ya kimataifa, PHEIC.
UNICEF yapeleka msaada China kusaidia waathirika wa virusi vya Corona wakiwemo watoto
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limepeleka msaada nchini China ili kusaidia kukinga maelfu ya watu wakiwemo watoto dhidi ya kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona
Virusi vya Corona vyathibitishwa na WHO kuwa vimeingia barani Ulaya
Jumamosi ya leo, Shirika la afya ulimwenguni limethibitisha kupitia ofisi yake ya kanda ya ulaya kuwa virusi vya Corona au 2019-nCoV ambavyo kwa majuma kadhaa sasa vimesababisha madhara makubwa nchini China, sasa vimethibitika nchini Ufaransa.