Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya Corona sasa vyatangazwa kuwa dharura ya kiafya ya kimataifa

Abiria wakiwa wamejikinga na maambukizi ya mfumo wa hewa wakiwa katika treni za chini ya ardhi huko Shenzhen China
UN News/Jing Zhang
Abiria wakiwa wamejikinga na maambukizi ya mfumo wa hewa wakiwa katika treni za chini ya ardhi huko Shenzhen China

Virusi vya Corona sasa vyatangazwa kuwa dharura ya kiafya ya kimataifa

Afya

Mkutano wa pili wa kamati ya dharura ulioitishwa hii leo mjini Geneva Uswisi na shirika la afya duniani, WHO, chini ya sheria za kimataifa za afya (IHR) (2015) kuhusiana na mlipuko wa virusi vya corona 2019-nCoV nchini China, umeutangaza mlipuko huowa virusi vya corona kuwa ni dharura ya kiafya ya kimataifa, PHEIC.

Wawakilishi wa Wizara ya afya ya China wameueleza mkutano huo kuwa hivi sasa kuna visa 7711 vilivyothibitishwa na kuna visa 12167 ambavyo vinahisiwa kuwa ni vya maambukizi ya virusi vya corona kote nchini China. 

Wataalamu hao wa afya wamesema kati ya visa vilivyothibitishwa, watu 1370 wako katika hali mbayá na tayari watu 170 wamefariki dunia.  Watu 124 wamepata nafuu na wameruhusiwa kutoka hospitali.

Dkt Tedros Ghebreyesus akizungumzia idadi ya waathirika amesema, "tunatakiwa kukumbuka kuwa hawa ni watu siyo tu namba." 

Tweet URL

 

 

 

 

Sekretarieti ya WHO imeeleza kuhusu hali ilivyo katika nchi nyingine ikisema kuwa kuna visa 82 katika nchi 18 hivi sasa. Na katika visa hivi vilivyopatikana katika nchi nyingine, 7 havina historia ya kusafiri kuiongia China. Kumekuwa na kuambukizana kati ya binadamu na binadamu katika nchi 3 nje ya China na mmoja wa wagonjwa hawa yuko katika hali mbayá lakini hakujatokea kifo chochote.

Dkt Tedros Ghebreyesus akijibu maswali ya wanahabari amesema kwa sasa hawajazuia watu wengine kusafiri kati ya China na nchi nyingine na pia China wamefanya juhudi kubwa kupambana na tatizo hilo akitolea mfano hospitali iliyojengwa ndani ya siku kumi, "na si hivyo pekee" amesisitiza. 

Mkutano wa kwanza ulikuwa umekubaliana kwamba japokuwa mlipuko wa virusi hivi unahitaji kushughulikiwa haraka lakini usingeweza kutangazwa kama dharura ya kiafya ya kimataifa. Hata hivyo katika mkutano wa leo na hususani baada ya tathimini ya nina na ya kitaalamu kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya visa vya maambukizi na usambaaji katika nchi nyingine, hatimaye sasa mlipuko huo ukatangazwa kuwa uko katika ngazi inayostahili kutangazwa kuwa dharura ya kiafya ya kimataifa.

Kamati imetambua kazi kubwa iliyofanywa na WHO na wadau, na pia juhudi zinazofanywa na serikali ya China.

Kamati pia imekiri pia kuwa bado kuna visa vingi ambavyo ahavijafahamika inagawa wanaamini kuwa bado kuana uwezekano wa kuzuia virusi hivyo kusambaa muhimu tu kwamba nchi ziweke hatua muhimu za kutambua ugonjwa huo mapema, kuwatenga katika maeneo maalumu na kuwatibu wagonjwa, kufuatilia walikotoka na waliokutana nao, na pia kutoa elimu kwa umma ili kujiepusha na hatari hiyo.

Aidha Kamati imesisitiza umuhimu wa kufuatilia kile kinachowezekana kuwa ni chanzo cha mlipuko huu wa virusi vya corona.

Abiria wakiwa wamejikinga na maambukizi ya mfumo wa hewa wakiwa katika treni za chini ya ardhi huko Shenzhen China
UN News/Jing Zhang
Abiria wakiwa wamejikinga na maambukizi ya mfumo wa hewa wakiwa katika treni za chini ya ardhi huko Shenzhen China

 

Kwa watu wa China

Mkurugenzi Mkuu ameeleza kwanza kuwa wamepokea maamuzi ya Kamati kuutangaza mlipuko huu wa virusi vya corona kuwa dharura ya kiafya ya kimataifa na akaeleza mapendekezo ya muda chini ya sheria za kimataifa za afya (IHR) (2015) kuwa pamoja na mambo mengine, watu wa China waendelee na hatua za kiafya za kuudhibiti mlipuko wa sasa, wahakikishe mnepo katika mfumo wa afya na pia kuilinda nguvu kazi ya huduma ya afya, waendelee kushirikiana na WHO na wadau kufchunguza na kuelewa chanzo na mabadiliko ya mlipuko huu na hatua za kuchukua na pia kusambaza kwa wataalamu taarifa na tatwimu za kina kuhusu visa vyote vya ugonjwa vinavyowakumba watu.

Kwa mataifa yote ulimwenguni

Kamati imeeleza kuwa kuna uwezekano wa ugonjwa kusambazwa kutokana na wasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa hivyo nchi zinatakiwa kujiandaa kwa kila namna kuweka miundombinu na utaalamu wa kutosha kufuatilia na kutibu ili kudhibiti ugonjwa huu kuenea zaidi.

Kamati hii ya dharura inategemewa kukutana tena ndani ya miezi mitatu au mapema kabla ya hapo, kutokana na uamuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO.