Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya Corona vyathibitishwa na WHO kuwa vimeingia barani Ulaya

Picha ya maktaba ikimwonesha mwanamke akikohoa katika kipande cha tishu au karatasi laini
WHO/J Sun
Picha ya maktaba ikimwonesha mwanamke akikohoa katika kipande cha tishu au karatasi laini

Virusi vya Corona vyathibitishwa na WHO kuwa vimeingia barani Ulaya

Afya

Jumamosi ya leo, Shirika la afya ulimwenguni limethibitisha kupitia ofisi yake ya kanda ya ulaya kuwa virusi vya Corona au 2019-nCoV ambavyo kwa majuma kadhaa sasa vimesababisha madhara makubwa nchini China, sasa vimethibitika nchini Ufaransa.

Taarifa hiyo ya WHO imeeleza kuwa visa vya kwanza vya virisi vya Corona vimeripotiwa  katika ukanda wa ulaya baada ya jana tarehe 24 Januari, Ufaransa kulitaariifu rasmi shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia afya ulimwenguni kote kuwa visa vitatu vya virusi hivyo vimethibitika nchini humo.

Wagonjwa wawili wamegundulika katika mji wa Paris na mwingine mmoja katika mji wa Bordeaux. Wagonjwa wote watatu walikuwa wamesafiri kutoka Wuhan, China na sasa wamelazwa katika hospitali nchini Ufaransa.

WHO imesema kwa hali ya kawaida ilivyo ya wasafiri, inategemewa maambukizi mengine yatasambazwa katika mataifa mengine na kunaweza kuwa na visa vingine katika ukanda wa ulaya.

Shirika hilo la afya limetoa wito kwa nchi katika ukanda wa ulayakujiandaa ikiwa virusi vipya vitasambazwa.