Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya kuhakikisha kuna mikakati endapo Virusi vya Corona vitazuka:WHO

Picha ya rangi ikionyesha seli ambayo imekumbwa na virusi vya MERS-Corona
National Institute of Allergy and Infectious Diseases, NIH, US
Picha ya rangi ikionyesha seli ambayo imekumbwa na virusi vya MERS-Corona

Kenya kuhakikisha kuna mikakati endapo Virusi vya Corona vitazuka:WHO

Afya

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeendelea kuzitaka nchi zote kuchukua tahadhari na kujiandaa dhidi ya virusi vya corona ambavyo tayari vimetangazwa kuwa dharura ya afya ya kimataifa vitazuka katika nchi zao.

Kitovu cha virusi hivyo kimekuwa mji wa Wuhan nchini Uchina ambako kwa mujibu wa WHO kuna jumla ya visa 9692 vilivyothibitishwa katika majimbo 31, na kati ya visa hivyo watu 1239 wako katika hali mbaya, 213 wamefariki dunia na wagonjwa 103 wametibiwa, kupona na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Na nje ya China kuna visa zaidi ya 68 vilivyothibitishwa katika nchi 18. Kenya nako kuna mgonjwa ambaye anafanyiwa uchunguzi ili kuthibitisha endapo ana virusi hivyo ama la? Ili kufahamu zaidi kuhusu Kenya Flora Nducha amezungumza na Dkt. Peter Borus afisa mtaalam wa masuala ya kisanyansi na dharura kwenye ofisi ya WHO Nairobi

(DR PETER BORUS)

"Virusi vya corona ni aina ya virusi vya homa lakini ni homa kali kidogo. Ni virusi vipya kwa sababu kwa kawaida, hivi sasa hivi virusi vinavyoripotiwa Wuhan, kule Uchina, ukiangalia vile maandishi yameandikwa, kuna herufi "N" mbele ya neno "Corona" hiyo ni kumaanisha "novel". Novel ni kitu kipya na tofauti. Hivi virusi ni vipya, wafanyikazi wa afya saa hizi wakiangalia, ni kitu tunachunguza kwa maana hakieleweki vizuri lakini  habari ambazo tumeanza kuangalia na kupata kutoka kwa wale ambao wamekwenda Uchina na kuhakikisha kwamba hali ya afya ya watu huko iko sawa, kuna hatari fulanai ambayo inahusikana na corona. Ingawa hizi sasa tumejua kwamaba haswa ni ya Uchina, na imaenea katika nchi kidogo hapa na pale, haijaeleweka vizuri hatari gani virusi hivi vinaweza kuleta"

Anapoulizwa kuhusu kisha chochote barani  Afrika, Dkt. Borus anasema

(DR PETER BORUS)

"Kama kawaida kwa usafiri wa ndege, kuna athari, magonjwa ya mfumo wa hewa yanakuwa na athari, nchi za Afrika kwa sabau ya kwenda Uchina amabyo inakuja Afrika, kwa hivyo athari bado iko" 

Na kuhusu mtu aliyesemekana kuwa na virusi vya corona nchini Kenya na tahadhari tunayopaswa kuchukua dhidi ya corona, anasema

(DR PETER BORUS)

"Uchunguzi bado unaendelea, mtu mwenyewe alipeleka katika hospitali ya Kenyatta hapa Nairobi. Sampuli imepelekwa kwa uchunguzi, na tunadhania kwamba kufikia kesho tutajua kama yuko ya ugonjwa huo kwa sababu alikuwa na joto mwilini, na makohozi kidogo na ni ambayo lazima ichunguzwe zaidi. Sanasana kwa sababu ni virusi vya kupumua na mtu anaweza kupata ugnojwa huo kutokana kikohozi, kujikinga kuna vifaa vinavyokubaliwa, kama unahisi kuna mtu anaugua huo ugonjwa, kuna vifaa unweza kuvaa ili usiambukizwe"

WHO inashirikiana vipi na nchi za afrika Mashariki na hasa Kenya katika maandalizi?

(DR PETER BORUS)

"WHO inashirikiana sana na serikali ya Kenya, tumekuwa kwa mikutano ya kuangalia ile mikakati ya kukinga. Tumepatiana mashauri mazuri ya kuangalia kwamba kwa wale ambiria ambao wanakuja, wanakaguliwa viti na ni vifaa vipi tunahitaji kukinga wafanyikazi wa afya ambao watakuwa wanahudumia hao wagonjwa. Tumekuwa na mikakati ya kuhakikisha ni vipi serikali itaweza kupeana habari kwa wananchi  bila kuhofisha watu. Watu wakihofia bila sababu, inaweza kuwadhuru. Tunashirikiana na serikali kuhakikisha kwamba habari amabyo inaelekea kwa wananchi ni habari ya ukweli, habari ambabyo haiwezi kudhuru watu. 

Nini ushauri wake kwa nchi na wananchi kuhusu virusi hivyo?

(DR PETER BORUS)

"Kitu cha muhimu ni serikali za nchi zikiwa na washikadau wao, waangalie kwamba wako na mikakati, na wameweka mpangilio ya kwamba vitu kama hivyo vikitokea, serikali zinaweza kuzuia kwa haraka sana ili isienee sana katika nchi. Wananchi wasiwe na hofu, wasiwe na taharuki, waangalie habari ambayo serikali inatoa, ile wizara ya afya inatoa, na wafuate hayo maagizo"