Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
COVID-19 imebadili maisha ya familia yangu- Mwanahabari Kanyinda
Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, upo na chonde chonde tujikinge. Ni kauli ya mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyoitoa baada ya kupona ugonjwa huo ulioenea katika mataifa 216 duniani.
Mbinu dhidi ya virusi vya Corona zachangia uhifadhi wa mazingira- UNEP
Naam na sasa tuelekee nchini Tanzania kusikiliza sehemu ya mchango au ushiriki wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19. Katika mahojiano haya yaliyofanywa na Hilda Phoya wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa UNIC Dar es salaam, Clara Makenya ambaye ni Mwakilishi wa UNEP nchini Tanzania anaanza kwa kueleza hatua zinazochukuliwa na shirika lake katika kupambana na COVID-19.
Mahojiano haya yameandaliwa na Hilda Phoya, UNIC Dar es salaam
Wakazi wa Nairobi wahaha kujinasua wakati huu wa janga la virusi vya Corona
Wakati ulimwengu bado unaendelea kutafakari ni kwa zipi utashinda vita dhidi ya virusi vya COVID-19, mamilioni ya watu wamejikuta kwenye hali ambayo hawakutarajia. Baadhi ya nchi za Afrika bado zinaendelea kushuhudia kuongeza kwa maambukizi ya virusi vya Corona. Kwa mfano nchini Kenya idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi suala ambalo limewatia hofu watu
Ulemavu alio nao mtoto huyu haukumzuia kusaka kipato kwa ajili ya familia yake
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, athari za janga la virusi vya Corona au COVID-19 zimekuwa mbayá zaidi kwa watoto wenye ulemavu, ambapo mtoto mmoja mkazi wa mji mkuu Kinshasa, ambaye ni kiziwi, amelazimika kusaka mbinu za kuweza kupata kipato ili kusaidia familia yake. John Kibego na maelezo zaidi.
Kinshasa, mji mkuu wa DR Congo katika video hii ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF yenye lengo la kuangazia sauti za vijana katikati ya janga la COVID-19, anaonekana Steve Okito, mtoto mwenye umri wa miaka 14.
Mtoto kiziwi alazimika kuosha magari jijini Kinshasa ili alee familia yake
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, athari za janga la virusi vya Corona au COVID-19 zimekuwa mbayá zaidi kwa watoto wenye ulemavu, ambapo mtoto mmoja mkazi wa mji mkuu Kinshasa, ambaye ni kiziwi, amelazimika kusaka mbinu za kuweza kupata kipato ili kusaidia familia yake.
Tanzania inavyokabili janga la corona
Ni miezi miwili na zaidi sasa tangu Tanzania itangaze mgonjwa wake wa kwanza wa virusi vya COVID-19. Tangu tarehe 16 mwezi wa tatu mwaka huu mengi yamejiri nchini Tanzania kufuatia kuzuka kwa janga la ugonjwa huo unaoathiri dunia nzima.
Serikali lazima ziwalinde wahamiaji wakati wa COVID-19
Wataalam wa haki za binadamu leo wametoa wito kwa serikali kulinda haki za wahamiaji na familia zao bila kujali hadhi zao za uhamiaji wakati na baada ya janga la virusi vya corona au COVID-19.
26 MEI 2020
Katika Jarida maalum la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea
-Walinda amani wawili wanawake mmoja kutoka Brazili na mwingine kutoka India wameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mchagizaji wa masuala ya kijinsia kwa mwaka 2019. Wanajeshi hao Meja Suman Gawani kutoka India na kamanda Carla Monteiro Araujo kutoka Brazili watakabidhiwa tuzo hiyo Ijumaa ya 29 Meisiku ya walinda amani duniani.
25 05 2020
Katika Jarida maalum la habari hii leo Flora Nducha anakuletea
Leo ikiwa ni siku ya Afrika Umoja wa Mataifa umelisihi bara hilo na nchi zinazofanya uchaguzi kudumisha demokrasia wakiendesha uchaguzi huo hata wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19
Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet, umebaini kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya koo na sababu kuu ikiwa ni uwepo wa mashine za uchunguzi zinazofanya uchunguzi kupita kiasi hususan katika nchi za kipato cha kati.
Afrika fanyeni chaguzi hata katika COVID-19
Umoja wa Mataifa umesihi nchi za Afrika ambazo zinatarajiwa kuwa na chaguzi zama hizi za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, zitekeleze hatua hiyo ya kidemokrasia ili kusongesha demokrasia na utulivu.