Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

World Bank/Arne Hoel

Wanandoa wakumbana na karaha badala ya raha, kisa? COVID-19

Katika mada kwa kina leo tunaelekea  Uganda, kumulika mizozo ya kifamilia wakati huu wa mlipuko wa COVID-19 na madhara yake. Mizozo ambayo inadaiwa kusababishwa na wanafamilia kukaa pamoja majumbani kwa muda mrefu kutokana na vizuizi vya kutembea vilivyowekwa na serikali ikiwa ni moja ya hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona. John Kibego anatupatia picha halisi.

Sauti
5'51"
Kambini Dadaab
UNHCR

COVID-19 yaingia katika kambi ya Dadaab, Kenya na UNHCR zaimarisha huduma ya afya katika kambi za wakimbizi

Baada ya wagonjwa wawili wa virusi vya corona kuthibitishwa katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hii leo limetoa taarifa kuwa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kutoa msaada wa kibinadamu pamoja na serikali ya Kenya wanaimarisha mapambano yao dhidi ya COVID-19 katika kambi za wakimbizi nchini humo.

Sauti
2'45"
MINUSCA

Guterres: Mshikamano na Afrika ni muhimu ili kusongesha maendeleo yaliyopatikana

Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ukiendelea kusambaa barani Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza hatua za kisera za  kusaidia bara hilo kukabiliana na changamoto zitokanazo na janga hilo ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu 2500 barani humo.

Guterres ametoa mapendekezo hayo kupitia andiko lake la kisera huku akipongeza jinsi Afrika imechukua hatua haraka akisema kuwa ingawa idadi ya vifo hivi sasa ni ndogo kuliko ilivyodhaniwa , bado kuna mambo mengi yamesalia.

Sauti
1'59"