Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Mafuriko, nzige na COVID-19 vyatishia kuirudisha nyuma Somalia:OCHA
Somalia taifa lililoghubikwa na miongo zaidi ya mitatu ya vita vinavyoendelea sasa mafuriko, nzige na janga la corona au COVID-19 vinatishia kurudisha nyuma hatua kubwa zilizopigwa za kisiasa na kiusalama, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misada ya dharura OCHA.
COVID-19 ni msumari wa tatu kwa wakimbizi na wahamiaji- Guterres
Janga la virusi vya Corona, COVID-19 likiendelea kuzua kizaazaa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tamko lake likitaka hatua zaidi kusaidia wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wahamiaji ambao amesema kwa makundi hayo janga hilo ni sawa na mwiba wa tatu katika majanga ambayo wanakumbana nayo.
02 June 2020
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo:
-Wahisani wa kimataifa wanakutana leo katika mkutano ulioitishwa na Ufalme wa Saudi ana Umoja wa Mataifa ili kuchangisha fedha kwa ajili hatua za kibinadamu kunusuru Maisha ya mamilioni ya watu nchini Yemen.
-Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet ametaka hatua za dharura zichukuliwe ili kukabilia na ubaguzi katika utoaji wa huduma dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona.
Ubaguzi wa kirangi katika kutibu COVID-19 ukome- Bachelet
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet ametaka hatua za dharura zichukuliwe ili kukabiliana na ukosefu wa usawa kwenye jamii unaosababisha ubaguzi katika utoaji wa huduma dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Wahisani wa kimataifa wakutana kuchangisha fedha kuinusuru Yemen:UN
Wahisani wa kimataifa wanakutana leo katika mkutano ulioitishwa na Ufalme wa Saudi ana Umoja wa Mataifa ili kuchangisha fedha kwa ajili hatua za kibinadamu kunusuru Maisha ya mamilioni ya watu nchini Yemen.
Nchi 30 na wadau wa kimataifa wajiunga kupiga jeki C-TAP:WHO
Nchi 30 na wadau mbalimbali wa kimataifa na taasisi wamejiunga kusaidia mkakati wa fursa za kiteknlojia dhidi ya janga la virusi vya corona au COVID-19 ujulikanao kama C-TAP, mkakati wenye lengo la kufanya chanjo, vipimo, matibabu na teknolojia zingine za kupambana na COVID-19 kupatikana kwa kila mtu, kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.
UNHCR inatoa tiba na ushauri nasaha kwa wakimbizi walioathirika na COVID-19 Colombia
Nchini Colombia katika mpaka na Venezuela shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linashirikiana na wadau kutoka huduma za tiba na ushauri nasaha kwa mamia ya watu walioathirika na virusi vya Corona au COVID-19 na huduma zingine, wakiwemo wakimbizi wa Venezuela waliovuka mpaka kuja kusaka msaada.
COVID-19 yadumaza tiba dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza- WHO
Huduma za kinga na tiba dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs zimevurugwa kwa kiasi kikubwa tangu kulipuka kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO kufuatia utafiti uliofanyika katika mataifa 155.
Wawili kati ya waliosafiri na ndege maalum ya UNAMID kutoka El Fasher,Sudan wakutwa na COVID-19 Nairobi
Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan, UNAMID umetangaza kuwa unashirikiana na mamlaka nchini Kenya kuwahudumia maafisa waliokutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Watu wawili wapoteza maisha na maelfu makazi yao baada ya moto kuzuka kambini Nigeria:UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wanaoneza juhudi za misaada kwa ajili ya watu 4,000 ambao ni wakimbizi wa ndani waliopoteza kila kitu katika moto mkubwa uliozuka na kuteketeza kambi ya wakimbizi wa ndani mjini Maiduguri jimbo la Borno Mashariki mwa Nigeria.