Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Je Barakoa ni mbadala wa kutochangamana?
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limetoa mwongozo mpya wa matumizi ya barakoa katika harakati za kuepusha maambukizi zaidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, hadi COVID-19 ilieleweke- UNMISS
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umezindua kampeni ya siku tano ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 kwenye maeneo manne yenye wakazi wengi zaidi eneo la Equatoria Magharibi.
Mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba hadi COVID-19 ilieleweke- UNMISS
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umezindua kampeni ya siku tano ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 kwenye maeneo manne yenye wakazi wengi zaidi eneo la Equatoria Magharibi.
COVID-19: IMF yasamehe deni la Tanzania la dola milioni 14.3, msamaha zaidi watarajiwa
Shirika la fedha duniani, IMF limeipatia Tanzania msamaha wa deni la dola milioni 14.3 ili kuwezesha nchi hiyo kuhimili athari zitokanazo na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
COVID-19: Maandalizi ya kuelekea “kawaida mpya” katika makao makuu ya UN
"Usalama na afya ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa nchi wanachama na wale wote ambao wanatumia jengo letu, ni kipaumbele cha kwanza. Kurejea kwa wafanyakazi jengoni kutazingatia mapendekezo ya jiji na jimbo la New York, ambayo watafuata kadri yatakavyokuja.” Atul Khare, Msaidizi wa Katibu Mkuu katika Operesheni.
Wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 Kenya kutibiwa nyumbani
Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 nchini Kenya ikifikia 300, serikali hii leo imetangaza mkakati wa kuepusha vituo vya afya na hospitali kuzidiwa uwezo wa kutibu wagonjwa hao.
Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna akizungumza jijini Nairobi, Kenya, amesema kuwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi watatibiwa hospitalini, lakini wale wasio na dalili zozote za ugonjwa wataugulia makwao.
10 JUNE 2020
Tenki za maji Mathare, Nairobi ni lulu katikati ya janga la COVID-19
Maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, yakiendelea kuripotiwa nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo limeanzisha zaidi ya vituo 1000 vya kunawa mikono katika eneo la makazi duni la Mathare kwenye mji mkuu Nairobi, kama njia mojawapo ya kukabiliana na maambukizi mapya.
Wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 Kenya kutibiwa nyumbani
Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 nchini Kenya ikifikia 3000, serikali hii leo imetangaza mkakati wa kuepusha vituo vya afya na hospitali kuzidiwa uwezo wa kutibu wagonjwa hao.