Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
UNICEF:COVID-19 kusababisha nyongeza ya watoto 6,000 kufariki dunia kila siku
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wiki hii linazindua kampeni iitwayo #Reimagine, yenye lengo la kuzuia janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, lisiwe janga la kudumu hususan kwa watoto walio hatarini zaidi kutokana na umaskini, kutengwa au ghasia majumbani. Ahimidiwe Olotu na taarifa zaidi
13 Mei 2020
Kampeni ya #Reimagine kuibuka na mpango wa dunia ya watoto baada ya COVID-19. Kitengo cha damu salama katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kimewatoa hofu wachangiaji wa damu kuwa uwepo wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 usiwatishe kwenda kuchangia damu. Katikati ya COVID-19, WFP yaendelea kunusuru wahitaji.
Jamii msiwe na hofu ya kuchangia damu wakati huu wa COVID-19, bado tunahitaji kuokoa maisha- Dkt Kitundya
Kitengo cha damu salama katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kimewatoa hofu wachangiaji wa damu kuwa uwepo wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 usiwatishe kwenda kuchangia damu kwani hawawezi kuambukizwa wala kuwaambukiza wengine kwa kuchangia damu.
COVID-19 kusababisha nyongeza ya watoto 6,000 kufariki dunia kila siku- UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wiki hii linazindua kampeni iitwayo #Reimagine, yenye lengo la kuzuia janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, lisiwe janga la kudumu hususan kwa watoto walio hatarini zaidi kutokana na umaskini, kutengwa au ghasia majumbani.
Katikati ya COVID-19, WFP yaendelea kunusuru wahitaji
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP, linaendelea kusaka rasilimali ili liweze kufikisha misaada kwa watu milioni 100 kwa mwaka huu 2020.
Ni wakati wa dini zote kushirikiana katika kupambana na COVID-19
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo kwa njia ya video amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu wa kidini duniani katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu jukumu la viongozi wa kidini katika kushughulikia changamoto za ugonjwa wa COVID-19.
WHO yasema vizuizi vya COVID-19 vikilegezwa, tujiandae kukabili changamoto
Idadi ya watu waliougua ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ikifikia zaidi ya milioni 4 duniani kote, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limesema kuwa hatua za baadhi ya nchi kulegeza masharti ya watu kubakia majumbani imeonesha baadhi ya changamoto zitakazokabili mataifa siku za usoni.
Hofu ya COVID-19 yaambatana na hofu ya ukatili majumbani huko Cox’s Bazar
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ingawa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, unakwamisha harakati za kufuatialia visa vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto katika kambi ya wakimbizi warohingya huko Bangladesh, bado kuna mbinu zinatumika kupatia msaada manusura.
Vizuizi vya COVID-19 vikilegezwa, tujiandae kukabili changamoto – WHO
Idadi ya watu waliougua ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ikifikia zaidi ya milioni 4 duniani kote, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limesema kuwa hatua za baadhi ya nchi kulegeza masharti ya watu kubakia majumbani imeonesha baadhi ya changamoto zitakazokabili mataifa siku za usoni.
‘Uharaka wa kuchukua hatua’ kwa ajili ya maendeleo endelevu, ni mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote wakati janga la corona likiendelea
COVID-19 ikiendelea inaendelea kuvuruga maisha na ustawi kote duniani, hii leo Jumatatu Umoja wa Mataifa umefanya mjadala mpana wa kisera kusisitiza suluhisho la ushirikiano wa kimataifa ili kupunguza janga wakati pia ulimwengu ukirejea katika mkondo wa kufikia Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu, SDGs.