Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

2 SEPTEMBA 2020

COVID-19 kuwatumbukiza wanawake wengine milioni 47 katika ufukara:UN Women/UNDP.  Familia zinazokimbia mashambulizi Msumbiji zajikuta katika maeneo yaliyoghubikwa na COVID-19.  IFAD imetuwezesha kujenga nyumba na kulala kwenye vitanda- Mkulima Ethiopia. 

Sauti
13'37"
Wakimbizi wa ndani katika maeneo ya Alto Gingone, Pemba mkoa wa Cabo Delgado, Msumbiji
UN Mozambique/Helvisney Cardoso

Familia zinazokimbia mashambulizi Msumbiji zajikuta katika maeneo yaliyoghubikwa na COVID-19 

Mashambulizi katika miji na vijiji vya mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado yamezidi na  kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia kwa miguu, boti au barabara kwenda katika makao makuu ya mkoa ambako ni kitovu cha COVID-19 na ambako shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC limesaidia kujenga kituo kikubwa cha matibabu kinachofunguliwa rasmi leo, imeeleza taarifa iliyotolewa hii leo na ICRC mjini Maputo. 

Sauti
2'31"

1 SEPTEMBA 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema muhula mpya wa masomo ukianza Agosti hadi Oktoba mwaka huu, theluthi moja ya wanafunzi bilioni 1 nukta 5 wa shule za awali hadi sekondari ndio wamejiandaa kurejea shuleni.Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na wadau wamekarabati na kukabidhi vyumba 16 vya huduma za dharura kwa ajili ya janga la corona au COVID-19 kwenye kituo cha wagonjwa mahututi mjini Yambio Magharibi mwa jimbo la Equatoria.  Mwalim

Sauti
12'24"
UNICEF/Shehzad Noorani

WHO:Huduma za afya zimevurugwa katika asilimia 90 ya nchi wakati wa COVID-19

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, leo limechapisha utafiti wake wa kwanza wa athari za janga la corona au COVID-19 kwa mifumo ya afya duniani. Hali ikoje? Loise Wairimu na taarifa zaidi.

Katika utafiti huo uliofanyika na takwimu kukusanywa katika nchi 105 duniani tangu mwezi Machi hadi Juni mwaka huu wa 2020, unaonyesha kuwa takriban asilimia 90 ya nchi hizo huduma zake za afya zimekabiliwa na changamoto huku nchi za kipato cha chini na cha wastani zikiarifu matatizo makubwa zaidi. 

Sauti
1'45"
Mama huko Mbarara, Uganda Magharibi, anahakikisha kuwa watoto wake wote wanapata dawa ARVs za watoto kwa wakati mmoja kila siku.
© UNICEF/Karin Schermbrucke

Ubia wa UNICEF na serikali Uganda waleta nuru kwa waishio na VVU 

Nchini Uganda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kwa kushirikiana na serikali, limechukua hatua kuhakikisha kuwa huduma za msingi za kiafya za kuokoa maisha ikiwemo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI zinapatikana hata wakati huu wa vizuizi vya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. 

Sauti
2'15"