Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Mwanafunzi wa kike nchini Ghana akinawa mikono kwa sabuni kabla ya kurejea darasani ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha elimu inaendelea huku wakidhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
UNICEF/Geoffrey Buta

Shule zikiwa zinaanza kufunguliwa, bado hakuna huduma za kujisafi kujikinga na COVID-19- Ripoti

Wakati huu ambapo shule katika maeneo mbalimbali duniani zikihaha kuanza tena mihula mipya baada ya karantini kutokana na janga la virusi vya Corona au COVID-19, ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa asilimia 43 ya shule kote ulimwenguni mwaka 2019 hazikuwa na huduma za msingi za kujisafi, ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, sharti ambalo ni la msingi kwa shule kuweza kuwa na mazingira salama kwa wanafunzi wakati huu wa janga la COVID-19.

Sauti
2'53"
Mpangilio wa ukaaji na pia ngao za kutenganisha kati ya mtu na mtu vimewekwa ili kuhakikisha umbali kati ya mtu na mtu katika hospitali mjini Bangkok, Thailand
ILO/Alin Sirisaksopit

Wagonjwa wa COVID-19 watafikia milioni 20 wiki hii-WHO 

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dkt Tedros Ghebreyesus ameueleza ulimwengu hii leo kuwa, wiki hii idadi ya wagonjwa wa COVID-19 walioathibitishwa itafikia milioni 20 na vifo 750,000 kote duniani  kwa hivyo viongozi wanatakiwa kuchukua hatua na raia wanatakiwa kuzifuata au kuzikumbatia hatua mpya.

10 Agosti 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
- Shirka la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda leo limesema limesikitishwa na kifo cha kwanza kabisa cha mkimbizi kutokana na virusi vya corona au COVID-19 tangu mlipuko huo utangazwe nchini humo mnamo Machi mwaka huu.
-Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaendelea na juhudi za kuokoa maisha Beirut 
- Watafiti wa malaria barani Afrika wameonya kuwa huenda bara hilo likajikuta katika hali ngumu ya kupambaan na ugonjwa wa malaria unao
Sauti
11'47"
Wizara ya Afya ya Bogotá imetuma muuguzi kwenda katika eneo la Suba, kaskazini mwa Bogotá , Colombia kuwahudumia watu wa jamii za asili.
PAHO/Karen González Abril

COVID-19 imekuwa na athari mbaya kwa zaidi ya watu wa asili milioni 476 kote ulimwenguni. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa njia ya video kuhusu siku ya leo ya watu wa asili ambayo huadhimishwa Agosti 9 ya kila mwaka, amesema  ni muhimu kwa nchi kuandaa rasilimali ili kushughulikia mahitaji ya watu wa asili, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao kujibu mahitaji yao, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao zisizopingika. 

UN/ John Kibego

COVID-19 Uganda yawa ‘mwiba’ kwa akina mama wanaonyonyesha watoto

Maziwa ya mama bado hayajathibitishwa kuwa na uwezo wa kuambukiza virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto," imesema WHO wakati huu ambapo kuna shaka na shuku kuwa yanaweza kusababisha maambukizi.

Wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama ikifikia ukingoni hii leo, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limesema kuwa bado hakuna uthibitisho wowote ya kwamba virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona, au COVID-19, vinaweza kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Sauti
1'56"