Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

1 SEPTEMBA 2020

1 SEPTEMBA 2020

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, limesema muhula mpya wa masomo ukianza Agosti hadi Oktoba mwaka huu, theluthi moja ya wanafunzi bilioni 1 nukta 5 wa shule za awali hadi sekondari ndio wamejiandaa kurejea shuleni.Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na wadau wamekarabati na kukabidhi vyumba 16 vya huduma za dharura kwa ajili ya janga la corona au COVID-19 kwenye kituo cha wagonjwa mahututi mjini Yambio Magharibi mwa jimbo la Equatoria.  Mwalimu mkimbizi ahofia kuwa fursa aliyopata ya kusoma ni finyu kwa wanae na watoto wengine wakimbizi.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'24"