Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 JULAI 2020

03 JULAI 2020

Pakua

Mada kwa kina inamulika lugha ya Kiswahili na ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini ambako walinda amani kutoka Tanzania wanahudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Wanafanya kazi kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi kilichoanzishwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2098  tarehe 28 mwezi Machi mwaka 2013. Mwenyeji wetu wa kutufafanulia uhusiano wa amani na lugha ya Kiswahili ni Luteni Issa Mwakalambo, Afisa habari wa kikosi cha Tanzania, TANZBATT 7. 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
9'58"