24 APRILI 2020

24 Aprili 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

-Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatiwa hofu na kamatakamata na kubanwa kwa vyombo vya habari wakati huu wa janga la COVID-19 ambapo taarifa sahihi ni muhimu sana

-Mkimbizi kutoka Katuza kutoka JJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC aneemeka na utengenezaji wa wanasesere kambini Msumbiji

Mada yetu kwa kina leo inaangazia unyanyapaa dhidi ya wagonjwa na washukiwa wa COVID-19 nchini Uganda

-Na katika kujifunza Kiswahili mchambuzi wetu Josephat Gitonga kutoka chuo kikuu cha Nairobi anafafanua maana ya methali "Ujana ni Moshi"

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
10'46"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud