Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutowaacha nyuma watoto wenye ulemavu ni kutimza mahitaji yao

Kutowaacha nyuma watoto wenye ulemavu ni kutimza mahitaji yao

Pakua

Elimu kwa wote ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu au SDGs ambalo linasisitiza usawa baina ya watoto wa kike na wa kiume katika kupata elimu bora lakini pia watoto wenye mahitaji maalum. Mkoani Songwe nchini Tanzania kuna shule ya watoto wenye mahitaji maalum lakini pamoja na kusoma kwenye shule maalum kuna changamoto lukuki zinazowakabili watoto hao ikiwemo miundombinu, vifaa na hata masuala ya msingi kama maji. John Kabambala kutoka Radio washirika TanzaniaKidsTime FM ametembelea shule hiyo kujionea hali halisi na kuzungumza na walimu na wanafunzi. Kwa undani zaidi ungana naye kwenye makala hii

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/John Kabambala
Sauti
3'43"
Photo Credit
© UNICEF/Pirozzi